19 WENGINE WATAJWA TAIFA STARS
Washambuliaji ni Athanas Mdamu
(Alliance), Haruna Chanongo (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis
Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga),
Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva
(Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Salum
Mayanga ametangaza wachezaji wengine 23 watakaoingia kambini kesho
(Aprili 20 mwaka huu) kuungana na 16 waliotajwa awali kujiandaa kwa
mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi
Manula (Azam), Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadili Ali (Azam). Mabeki
ni Abdi Banda (Coastal Union), Aidan Michael (Ruvu Shooting), Aggrey
Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City),
Kelvin Yondani na Said Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Frank Domayo (Yanga), Himid Mao (Azam) na Jonas Mkude (Simba).

Wachezaji walioitwa kutoka katika kikosi
cha maboresho ni kipa Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara), mabeki wa kati;
Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi
wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga
(Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).
Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili
(Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed
(Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani
Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).
Washambuliaji ni Mohammed Seif Saidi
(Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally
(Mjini Magharibi), Paul Michael Bundara (Ilala). Wachezaji wa U 20 ni
Mbwana Mshindo Musa (Tanga) na Bayaga Athanas Fabian (Mbeya).
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach.
MICHUANO YA BEACH SOCCER YAIVA
Michuano ya mpira wa miguu ya ufukweni
(Beach Soccer) inazinduliwa rasmi kesho (Aprili 20 mwaka huu) kwenye
ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni, Dar es Salaam na kushirikisha
timu 13.
Uzinduzi huo utaanza saa 5 asubuhi na
mechi zitachezwa hadi saa 11 jioni. Michuano hiyo inayofanyika kwa mara
ya kwanza nchini inashirikisha timu 13 kutoka vyuo mbalimbali vya jijini
Dar es Salaam.
Vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha Ardhi (AU),
Chuo Kikuu cha St. Joseph Tanzania (SJUIT), Chuo Kikuu cha Tumaini Dar
es Salaam (TUDARCO), Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW), Chuo cha Uandishi
wa Habari Dar es Salaam (DSJ) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Vingine ni Chuo cha Utumishi wa Umma
Magogoni, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Elimu ya Biashara
(CBE), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Taasisi ya Uhasibu
Tanzania (TIA), Chuo cha Utawala wa Kodi (ITA) na Chuo cha Taifa cha
Usafirishaji (NIT).
Michuano hiyo itakuwa inachezwa Jumamosi
na Jumapili kwenye fukwe za Escape One na Gorilla Beach iliyopo
Kigamboni, Dar es Salaam.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)