Wednesday, April 24, 2013

AJIWEKA PEMBENI KAMATI YA FIFA
MJUMBE wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Nicolas Leoz kutoka Paraguay amejiuzulu wadhifa wake huo kutokana na kile alichodai kuwa na matatizo ya kiafya ikiwa ni siku chache kabla ya shirikisho hilo halijatangaza uchunguzi wa bakshishi katika michuano ya Kombe la Dunia. FIFA ilithibitisha kupokea barua ya Leoz mwenye umri wa miaka 84 ambaye pia ataachia ngazi wadhifa wake wa urais wa Shirikisho la Soka la Amerika Kusini-CONMEBOL. Leoz ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo mara kadhaa amekuwa mjumbe katika bodi ya FIFA kuanzia mwaka 1998 na amekuwa rais wa CONMEBOL kuanzia mwaka 1986. Katika barua yake Leoz amesisitiza kuwa uamuzi aliochukua ni binafsi kutokana na matatizo ya kiafya aliyonayo kwani hawezi kusafiri mara tano kwa mwaka kama ilivyokuwa zamani.


Ijapo kuwa matajiri wa london Man city wameonekana kuvutiwa na kiwango chake KLABU ya Paris Saint-Germain-PSG ya Ufaransa imemtengea mkataba mnono wa euro milioni 8.5 kwa msimu mshambuliaji nyota wa Napoli ya Italia Edinson Cavani. Imeripotiwa na vyombo vua habari nchini humo kuwa mkurugenzi wa michezo wa klabu ya PSG, Leonardo ameshafanya vikao kadhaa na wakala wa nyota huyo kuzungumzia uhamisho wake kutoka Napoli ambao unakaribia kufikia kiasi cha euro milioni 63. Mbali na PSG vilabu vingine vikubwa barani Ulaya ambavyo vimeonyesha nia ya kuhitaji sahihi ya nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay ni pamoja na Real Madrid, Manchester City na Chelsea. Cavani mwenye umri wa miaka 26 ana mkataba na Napoli mpaka 2015 ambao unamuwezesha kulipwa kiasi cha euro milioni 1.4 kwa msimu.