VYOMBO vya habari katika nchi ya Brazil vimerioti kuwa mashabiki wawili wa soka nchini humo wamepigwa
risasi na kufa wakati wakielekea katika Uwanja wa Castelao Arena uliopo
katika mji wa Fortaleza. Kwa
mujibu wa taarifa hizo mashabiki hao walikuwa wakielekea kuishangilia
timu ya Ceara ambayo ilikuwa ikicheza na wenyeji Fortaleza kabla ya
vijana hao kuanzisha vurugu kwa kuwarushia mawe wapinzani wao ambao nao
walijibu mapigo na kupelekea vifi vyao. Taarifa
hizo ziliendelea kudai kuwa tukio hilo lilitokea maeneo ya karibu na
uwanja huo ambao ni mojawapo ya viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya
michuano ya Kombe la Dunia 2014. Katika mchezo huo ambao ulizua tafrani hiyo Ceara walifanikiwa kuwafunga mahasimu wao Fertaleza kwa bao 1-0.v