BINGWA mara mbili wa
dunia mashindano ya mbio ndefu Abel Kirui na mshindi wa medali ya shaba
katika michuano ya olimpiki Wilson Kipsang wamejitoa katika timu ya
wanariadha ya Kenya itakayoshiriki michuano ya riadha ya dunia
itakayofanyika jijini Moscow. Makamu
wa rais wa Chama cha Riadha cha nchi hiyo Paul Mutwii amedai kuwa Kurui
aliwafahamisha kwamba amejitoa kwasababu ya kusumbuliwa na majeraha
wakati Kipsang yeye amewaambia kuwa ana majukumu mengine. Kirui
ambaye alishinda taji la dunia la mbio ndefu mwaka 2009 na 2011 amekuwa
akisumbuliwa jeraha la kifundo cha mguu wake wa kulia na anatarajiwa
kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita. Kuziba
nafasi hizo Mutwii amesema wamewaita Mike Kipyego ambaye alishinda mbio
za marathon jijini Tokyo mwaka jana, Bernard Kipyego mshindi wa medali
ya fedha mbio za nusu marathon 2009 na bingwa wa mbio za marathoni za
Paris Peter Some. Kikosi cha mwisho kitakachokwenda Moscow kitatajwa mwezi ujao baada ya kufanyika mbioza mchujo.