
Bolt amekuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia chini ya sekunde 20 katika mbo za mita 200 msimu huu aliwasili jiji Oslo baada kushindwa na Justin Gatlin katika mbio za mita 100 zilizofanyika jijini Rome wiki iliyopita. Baadae Bolt aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa ingawa kulikuwa na baridi sana lakini alijitahidi kukimbia kwa kasi kadri alivyoweza na kama alivyoahidi hivyo anashukuru kwa kufanya vyema. Mshindi wa pili katika mbio hizo alikuwa ni Jasyma Saidy Ndure wa Norway huku mshindi wa tatu akiwa James Ellington wa Uingereza.