
Vyama
vya mikoa Lindi na Dar es Salaam na Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake
(TWFA) viliomba kuongezewa muda wakati vingine vimeomba Katiba mama kama
angalizo lao la mabadiliko hayo. Klabu ya Simba Sports ndiye mwanachama
pekee aliyewasilisha mabadiliko ya Katiba. TFF inawapongeza viongozi na
wanachama wa klabu hiyo kwa kufanya mkutano wao kwa utulivu.
Kamati
itatangaza nyongeza ya muda wa kufanya mabadiliko hayo baada ya kuviandalia
vyama vya mikoa na vyama shiriki katiba mfano kwa ajili ya kurahisisha shughuli
hiyo.
Baada
ya kupitia uamuzi wa wanachama wa Simba S.C. Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji imeamua ifuatavyo:
(i)
Kwa kuwa pendekezo la wanachama wa Simba kubadili kipengele na 26 kuhusu sifa
za mgombea kinapingana na kipengele na 29 (4) cha Katiba ya TFF, hivyo
basi Kamati imeagiza kipengele cha Katiba ya Simba kibaki vilevile bila
kubadilishwa.
(ii)
Vipengele vingine vyote vimepitishwa na vitapelekwa kwa Msajili wa Klabu
na Vyama vya Michezo kwa ajili ya kusajiliwa.
(iii)
Mchakato wa uchaguzi wa Klabu ya Simba uendelee kama ulivyopangwa wakizingatia
uamuzi huu wa Kamati. TFF inaitakia Klabu ya Simba uchaguzi mwema.
Pia
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imeshauri TFF kuwasiliana na FIFA kupata
mwongozo kuhusu katazo la watu wenye rekodi ya kifungo kugombea.
TFF
imepokea ushauri huo na itaufanyia kazi na kama kuna mabadiliko yoyote
kiutaratibu yataanzia katika Katiba ya TFF kupitia Mkutano Mkuu.
RAMBIRAMBI
MSIBA WA DK HEMED MZIRAY
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha daktari wa
tiba ya michezo, Dk. Hemed Mziray kilichotokea juzi jijini Dar es Salaam.
Dk.
Mziray ambaye alikuwa mfanyakazi wa Hospitali ya Manispaa ya Temeke na mjumbe
wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Tiba ya Michezo Tanzania (TASMA)
amesafirishwa kwenda kwao mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.
Msiba
huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Dk.
Mziray ameshirikiana na TFF na wadau wengine wa mpira wa miguu katika masuala
ya tiba na uongozi.
Alikuwa
kiungo kati ya Uwanja wa Taifa ambapo mechi za kimataifa, za ligi na za
kirafiki zimekuwa zikichezwa na Hospitali ya Temeke kwa wagonjwa wanaohitaji
huduma zaidi, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Dk. Mziray, TASMA na wafanyakazi wa
Hospitali ya Temeke na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki
kigumu cha msiba huo mzito. Pia TFF inatoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya
marehemu kama rambirambi zake.
Bwana
alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina
MECHI
YA AZAM, SIMBA YAINGIZA MIL 26/-
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana (Machi 30
mwaka huu) Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imeingiza sh. 26,455,000.
Mgawanyo
kwa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 4,035,508.47, gharama
za kuchapa tiketi sh. 3,908,686 wakati kila klabu ilipata sh. 5,460,687.63.
Uwanja
sh. 2,776,620.83, gharama za mechi sh. 1,665,972.50, Bodi ya Ligi sh.
1,665,972.50, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 832,986.25 na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 647,878.19.