SUAREZ AFUNGUKA KUWA INIESTA ALISTAHILI TUZO YA BALLON D"OR MWAKA 2010
Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez anaamini kuwa Andres Iniesta alistahili kushinda
tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2010 zaidi kuliko mshindi wa tuzo hiyo Lionel
Messi. Messi ambaye alishinda tuzo hiyo kwa miaka minne mfululizo,
alinyakuwa tuzo hiyo mwaka 2010 mbele ya wachezaji wenzake wa Barcelona
Iniesta na Xavi Hernandez pamoja na wenzake hao kunyakuwa taji la Kombe
la Dunia wakiwa na timu ya taifa ya Hispania pamoja na taji La Liga
wakiwa na klabu yao. Lakini Suarez ambaye ni Mhispania pekee kunyakuwa
tuzo hiyo anadhani Xavi na Iniesta ambaye alifunga bao la ushindi katika
mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia alitakiwa kuwa mbele ya Messi
aliyepewa tuzo hiyo. Suarez amesema katika miaka ya karibuni Hispania
imeuwa ikifanya mambo mengi muhimu na mchezaji yoyote wan chi hiyo
anastahili kushinda Ballon d’Or. Nguli huyo ambaye hivi sasa ana umri wa
miaka 78 aliedelea kudai kuwa La Liga pia ina wachezaji wawili wa
kiwango cha juu kabisa Messi na Cristiano Ronaldo lakini anafikiri mwaka
ambao Hispania walitawadhwa mabingwa wa dunia Iniesta au Xavi
walistahili tuzo ya Ballon d’Or.