Timu
ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Tanzania, Ngorongoro
Heroes imejiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye Fainali za
Afrika mwakani nchini Senegal, baada ya kulazimisha sare ya bila
kufungana na Kenya Uwanja wa Kenyatta, Machakos nchini Kenya jana
katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza. Ngorongoro sasa inahitaji
hata ushindi wa 1-0 katika mchezo wa marudiano Dar es Salaam ili kusonga
mbele. katika mchezo vijanawa Heroes wameonekana kabisa kuwa wana kiu ya kwenda senegal mwakani baaa ya kutandaza soka la nguvu lenye kuvutia mbele ya vijana wa kenya.