Saturday, April 19, 2014

SIMBA YANGA HAKUNA MBABE AZAM YAKABIDHIWA NDOO.

Goli la dakika ya 86 la Simon Msuva dakika ya 86, jioni hii limeinusuru Yanga SC kulala mbele ya wapinzani wake, Simba SC baada ya kupata sare ya 1-1 katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Uwanja wa Azam Complex, Chamazi bao la Brian Umony limeipa Azam ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Ruvu.

Simba SC ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Haroun Chanongo dakika ya 68 na kwa matokeo hayo, Azam inamaliza Ligi Kuu na pointi 62 wakati Yanga SC inamaliza na pointi 56 katika nafasi ya pili- ambapo sasa Azam FC ni mabingwa wapya ambao hawaja poteza mechi hata moja katika msimu wa Ligi Kuu  2013/2014.

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ameikabidhi mkabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni hii baada ya kuifunga bao 1-0 JKT Ruvu Uwanja wa Azam C
omplex, Chamazi, Dar es Salaam.


Mabingwa hao wakisherehekea na taji lao ambapo sherehe za ubingwa zimeanza jioni hii katika uwanja wa  Complex hadi usiku wa mana
ne

Mbali ya yotetimu zilizoshuka daraja msimu huu ni Ashanti United, Jkt Oljoro Pamoja na Rhino Rangers ambazo zimeaga mkono wa
kwaheri kuzipisha timu za Stends United ya shinyanga,Polisi Morogoro Pamoja na Ndanda fc ya Mtwara.