Coastal
union ambayo imemaliza Ligi Kuu Bara ikishika
nafasi ya tisa na alama 29 ambapo ilikuwa sio matarajio ya wanachama wa club
hiyo nao wametoa neno.
Wanachama
ambao wa club hiyo kutoka jiji la Tanga walitoa ujumbe kwa uongozi wao
wakionyesha kupinga mambo kadhaa yanayoonekana kutokwenda sawa.
Lakini
kilichoonyesha kweli mambo hayo hayako vizuri ni wachezaji kwenda kuwaunga
mkono wanachama hao mara baada ya mechi hiyo kwisha.
Uongozi
wa Coastal Union, umekuwa ukishutumiwa kukataa kutoa kadi mpya za wachama, huku
Kassim El Siagi ambaye ni katibu mkuu akielezwa kuwa chanzo.
Siagi
amekuwa akisisitiza kwamba lazima kabla ya kuwakubali wanachama wapya, basi
wawahakiki kwanza kwa kuwajadili.
Lakini
katiba ya Coastal Union haina kipengele hicho.