Friday, May 16, 2014

BALE ASEMA RONALDO NI MTU POA SANA

Mchezaji Mahiri Gareth Bale ameweka wazi na kusema kuwa Mchezaji mwenzake wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ni Mtu mwema sana tofauti na baadhi ya Watu wanavyomchukulia.
Bale alijiunga Real Madrid akitokea Tottenham Mwaka Jana kwa Dau la Euro Milioni 100 likipiku Dau la Ronaldo aliponunuliwa toka Man United la Euro Milioni 94.
Hata hivyo, Bale, Raia wa Wales, amesisitiza Ronaldo alimkaribisha vyema Jijini Madrid na ametamka: “Tangu nifike hapa amekuwa Mtu wa ajabu kwa kunisaidia ndani na nje ya Uwanja. Ni Mtu mwema, anasaidia sana, na Siku zote anataka Timu ishinde lakini Watu wanaandika tofauti!”
Bale pia amekiri Luka Modric, ambae walikuwa nae Tottenham na kuhamia
Real Mwaka mmoja kabla, amekuwa mkarimu sana kwake.
Bale ameeleza: “Tulikuwa na Luka Miaka mitano Spurs na tulikuwa na uhusiano mzuri sana na hili limenisaidia nilip
okuja hapa. Yeye alitua hapa hamjuia Mtu na ilikuwa ngumu kwake. Lakini nilipokuja mimi nimemkuta yeye na nilifarijika sana.”
Bale pia amesema kuwepo kwa Watu maarufu kama kina Zinedine Zidane, ambae yupo chini ya Meneja wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, kumemwinua sana.
Mbali ya kuisaidia Real Madrid kutwaa Copa del Rey Msimu huu baada ya kufunga Bao la Pili, la ushindi na la ajabu dhidi ya Barcelona Mwezi uliopita, Bale pia ana nafasi kubwa hapo Mei 24 kutwaa Ubingwa wa Ulaya wakati Real Madrid itakapokutana na Atletico Madrid huko Lisbon, Ure
no kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIOZ LIGI.