SHIRIKISHO
la soka Tanzania limeshauriwa kutokata tamaa na mpango wake wa
maboresho ya Taifa Stars kupitia mkakati wake wa kusaka vipaji mikoani
ulioanzishwa hivi karibuni.
Taifa
stars ya maboresho iliweka kambi mjini Tukuyu mkoani Mbeya na kwa mara
ya kwanza ilionekana aprili 26 mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi kuadhimisha miaka 50 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mechi
hii iliyowavutia wadau wengi wa soka kwa lengo la kuona vipaji vipya
kutoka mikoani, Stars ilifungwa bao(3-0).
Taifa
Stars ilikuwa imesheheni vipaji vipya vilivyopatikana katika mkakati wa
maboresho ya Taifa stars ambapo jopo la makocha waliteuliwa na TFF na
kuzunguka nchi nzima kusaka vijana wa kuingizwa katika timu.
Wakati
mkakati huu ukitangazwa, wadau waliuchukuliwa kwa mitazamo miwili
tofauti ambapo na kundi moja liliunga mkono na lingine likapinga kwa
madai kuwa hautakuwa na tija kwa wakati huu ambao timu inajiandaa kufuza
AFCON mwakani nchini Morocco.