Tuesday, November 4, 2014

RASMI:KALI ONGALA WA AZAM FC ACHIA NGAZI KUIFUNDISHA TIMU HIYO

Kocha msaidizi wa azam Fc kali Ongala ameachia ngazi kuifundisha klabu hiyo kwa sababu ya kwenda nchini England kuendelea na masomo.
Jafari iddy Maganga Ofisa Habari wa klabu hiyo amesema kocha huyo amekuwa akishiriki kozi fupi fupi za ukocha kwa muda mrefu nchini humo,lakini sasa ameamua kuomba uongozi wa klabu hiyo muda mrefu wa kwenda kasoma masomo hayo yatakayochukuwa muda mrefu.
Jaffari iddy amekanusha taarifa za kocha huyo kuachia ngazi kwa sababu ya kutoelewana na klabu hiyo baada ya matokeo yasiyolizisha.
Kali alisajiliwa mwaka 2009 kama mchezaji wa ndani akitokea nchini Sweden na baadaye aliondoka nchini Uingereza kwa ajili ya kusomea ukocha na kurejea akiwa kocha msaidizi wa timu hiyo.