Thursday, April 18, 2013

WAARABU WAJA NA VITUKO KEDEKEDE


TIMU ya AS FAR Rabat ya Morocco itakayoikabili Azam kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho imetua jana (Aprili 17 mwaka huu) saa 7.30 mchana kwa ndege ya Qatar Airways.

Wapinzani hao wa Azam FC katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, AS FAR Rabat ya Morocco baada ya kuwasili jana Dar es Salaam wameanza na vituko kedekede.
kwanza wamijawa na  wasiwasi tangu wanatua katika dimba la Uwanja wa Ndege na kutoa imani kwa  wapinzani wao, wakikataa mapokezi na mwishowe  kukataa hoteli waliyokodiwa na wenyeji wao, Sapphire Court.
Pamoja na kuambiwa hoteli hiyo imepitishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na timu zote zilizocheza na Azam katika mashindano hayo, zilifikia hapo, Al Nasir ya Sudan Kusini na Barack Young Controllers II ya Liberia, lakini wakagoma.
Wenyeji wakawaambia kama hawataki hoteli hiyo watajilipia popote watakapokwenda na Waarabu hao nao wakaonyesha jeuri ya fedha kwa kujipangia New Africa Hotel. Kaazi kweli kweli.
ukitafakari kwa undani zaidi ni moja ya dalili mbaya kwa Waarabu hao kugomea hoteli na visa vyote walivyofanya, hata hivyo ni hatari kwa Azam  katika wakielekea  Morocco kwa ajili ya mchezo wa marudiano.
Azam watakwatuana na timu hiyo ya far rabat {Waarabu hao} Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Tatu, kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye Morocco na mshindi wa jumla ataingia kwenye droo ya kucheza na timu zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho. 
Azam FC ilifanikiwa kuingia Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, baada ya kuichalaza magoli 2-1 Barack Young Contollers II ya Liberia.Ilianza kwa kushinda 2-1 mjini Monrovia kabla ya kulazimishwa sare ya bila kufungana Dar es Salaam.

Tuesday, April 16, 2013

KAMATI  MAALUM YAUNDWA KUHUSU TAIFA STAR "

SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo imeunda kamati maalumu kwa ajili ya kuisaidia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ili iweze kufanya vizuri kwenye michezo yake iliyobakia ya kufuzu michuano ya Kombe la dunia 2014. Hivi karibuni Stars ilifanikiwa kuitandika Morocco mabao 3-1 hivyo kufanikiwa kujiweka katika nafasi nzuri kwenye kundi C walilopo wakiwa na timu zingine za Ivory Coast na Gambia. Msimamo wa kundi hilo mpaka sasa Stars wako katika nafasi ya pili wakiwa na point sita, nyuma ya vinara Ivory Coast wanaoongoza kwa alama saba na Morocco ni ya tatu wakiwa na alama mbili wakati Gambia wao wanashikilia mkia wakiwa na alama moja. Kutokana na matokeo hayo wizara kupitia waziri wake Fenela Mukangara wameipongeza timu hiyo kwa kuweka matumaini hai ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil 2014. na kwa kuzingatia hilo wizara imeamua kuunda kamati maalumu kwa ajili ya kuongeza hamasa ya ushindi kwa Stars ili iweze kuweka historia kwa kushiriki michuano ya Brazil. Jukumu la msingi la Kamati iliyoundwa ni kuhakikisha Taifa Stars inawezeshwa na kuandaliwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuunda kikundi cha kuishangilia timu ya Taifa ndani na nje ya nchi.star kwa sasa katika viwango vya fifa ipo katika nafasi ya 116

Wajumbe wa Kamati ya Taifa Stars Stars itakayoongozwa na Mhe. Mohamed Dewji ni hawa wafuatao:-


Mhe Mohamed Dewji - Mbunge
Bi. Teddy Mapunda - Montage
Dkt. Ramadhani Dau - Mkurugenzi Mtendaji NSSF
Bw. Dioniz Malinzi - Mwenyekiti BMT
Bw. Abji Shabir - New Africa Hotel
Bw. George Kavishe - TBL
Mhe. Mohamed Raza - Zanzibar
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Bw. Joseph Kusaga - Clouds
Mhe. Kapt. John Komba - Mbunge
Mhe. Zitto Kabwe - Mbunge
Kamati hiyo iliyoteuliwa leo, inatakiwa kuanza kazi kazi mara moja. Hadidu za rejea zitakazowaongoza kutekeleza majukumu yao chini ya Kamati hii watazipata kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kamati itashirikisha wadau mbalimbali kadri itakavyoona inafaa. Serikali inaahidi kutoa ushirikiano utakaohitajika katika kuhakikisha Kamati hii inafanya kazi vizuri ili kuiwezesha Taifa Stars kushinda Mechi zote zilizombele yetu.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TFF_LOGO12Aprili 16, 2013
RAMBIRAMBI MSIBA WA MEJA JENERALI MAKAME RASHID
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko za kifo cha Mkuu wa zamani wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Makame Rashid kilichotokea juzi (Aprili 14 mwaka huu) kutokana na maradhi jijini Dar es Salaam.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kutokana na mchango aliotoa Meja Jenerali Makame Rashid ikiwemo kuwa mlezi wa timu ya Ruvu Stars wakati huo akiwa Kamanda (CO) wa Kikosi cha Ruvu JKT.
Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mdhamini (Trustee) wa TFF wakati huo ikiitwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) na wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika miaka ya themanini alikuwa sehemu ya mafanikio kwa timu ya Tukuyu Stars ya Mbeya iliyotwaa ubingwa wa Tanzania Bara mwaka 1987 ikiwa ndiyo kwanza imepanda kucheza Ligi Kuu wakati huo ikiitwa Ligi Daraja la Kwanza.
TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Meja Jenerali Makame Rashid, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Maziko yanatarajiwa kufanyika leo (Aprili 16 mwaka huu) nyumbani kwao mkoani Mtwara. Mungu aiweke roho ya marehemu Sembwana mahali pema peponi. Amina
VPL KUTIMUA VUMBI VIWANJA VITATU
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Aprili 17 mwaka huu) kwenye viwanja vitatu huku vinara wa ligi hiyo Yanga wakifukuzia ubingwa huo jijini Tanga.
Yanga inayoongoza ligi ikiwa na pointi 52 itakuwa mgeni wa Mgambo Shooting katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Athuman Lazi kutoka Morogoro kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Waamuzi wasaidizi wa mechi hiyo ni Michael Mkongwa wa Iringa na Godfrey Kihwili wa Arusha wakati Kamishna wa mechi hiyo ni Godbless Kimaro kutoka Moshi.
Kagera Sugar na Toto Africans zitaumana kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba katika mechi namba 164 itakayokuwa chini ya mwamuzi Martin Saanya wa Morogoro.
Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro, na wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 4,000 utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mtibwa Sugar yenye pointi 33 na Oljoro JKT yenye pointi 28.
Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam ndiye atakayechezesha mechi hiyo akisaidiwa na Hamis Chang’walu (Dar es Salaam) na John Kanyenye (Mbeya). Kamishna wa mechi hiyo ni Ramadhan Mahano kutoka Iringa.
AS FAR KUWASILI KESHO KUIKABILI AZAM
Wapinzani wa Azam katika michuano ya Kombe la Shirikisho, AS FAR Rabat ya Morocco wanatarajiwa kutua nchini kesho (Aprili 17 mwaka huu) saa 7 mchana kwa ndege ya Emirates.
Msafara wa timu hiyo wenye watu 28 utafikia hoteli ya Sapphire iliyoko maeneo ya Kariakoo, Dar es Salaam tayari kwa mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itakayochezwa Jumamosi (Aprili 20 mwaka huu) saa 10 kamili jioni Uwanja wa Taifa.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Monday, April 15, 2013

TAARIFA ZA MAPATO KUTOKA TFF LEO.

MECHI YA AZAM, SIMBA YAINGIZA MIL 66/-
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana (Aprili 14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 66,855,000 kutokana na watazamaji 11,458. Viingilio katika mechi hiyo namba 155 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,587,177.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,198,220.34. Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,925,683.45, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,755,410.07, Kamati ya Ligi sh. 4,755,410.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,377,705.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,849,326.14.



WATAZAMAJI 11,021 WAZISHUHUDIA YANGA, OLJORO
Watazamaji 11,021 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Oljoro JKT iliyochezwa juzi (Aprili 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 63,170,000. Viingilio katika mechi hiyo namba 156 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,853,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,636,101.69. Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,552,501.25, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,531,500.75, Kamati ya Ligi sh. 4,531,500.75, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,265,750.37 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,762,250.29.
MASHABIKI WAWILI NCHINI BRAZIL WAUWAWA
VYOMBO vya habari katika nchi ya Brazil vimerioti kuwa mashabiki wawili wa soka nchini humo wamepigwa risasi na kufa wakati wakielekea katika Uwanja wa Castelao Arena uliopo katika mji wa Fortaleza. Kwa mujibu wa taarifa hizo mashabiki hao walikuwa wakielekea kuishangilia timu ya Ceara ambayo ilikuwa ikicheza na wenyeji Fortaleza kabla ya vijana hao kuanzisha vurugu kwa kuwarushia mawe wapinzani wao ambao nao walijibu mapigo na kupelekea vifi vyao. Taarifa hizo ziliendelea kudai kuwa tukio hilo lilitokea maeneo ya karibu na uwanja huo ambao ni mojawapo ya viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2014. Katika mchezo huo ambao ulizua tafrani hiyo Ceara walifanikiwa kuwafunga mahasimu wao Fertaleza kwa bao 1-0.v

Saturday, April 13, 2013

YANGA YAINYUKA OLJORO 3- MTUNGI HATIMAYE YAIVUA UBINGWA SIMBA""
KATIKA  dimba la Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga wameitandika JKT Oljoro kwa Bao 3-0 na kuzidi kukwea kileleni mwa VPL, Ligi Kuu Vodacom, wakiwa Pointi 6 mbele ya Timu ya Pili Azam FC.

Ushindi wa leo pia umeivua rasmi Simba Ubingwa kwa vile wana Pointi 35 na wamebakiza Mechi 5 na hata wakishinda zote watafikisha Pointi 50 ambazo Yanga wameshazipita.
WAFUNGAJI
MAGOLI:
-Dakika ya 5 Nadir Haroub ‘Cannavaro’
-Dakika ya 19 Simon Msuva
-Dakika ya 43 Hamis Kiiza
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
VPL itaendelea kesho Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa bigi mechi kati ya Simba na Azam FC na kipigo kwa Azam FC kitaipa nafasi Yanga kutwaa Ubingwa.
MATOKEO VPL LEO


Yanga 3-0 Jkt oljoro
T/prison 2-0 Ruvu shooting


MSIMAMO:
NA
TIMU
p
W
D
L
GD
PTS
1
YANGA
21
15
4
2
28
52
2
Azam FC
23
14
4
4
22
47
3
Kagera Sugar
22
10
7
5
7
37
4
Simba
22
9
8
4
12
36
5
Mtibwa Sugar
23
8
9
6
2
33
6
Coastal Union
22
8
8
6
3
32
7
Ruvu Shooting
21
8
6
7
2
30
8
JKT Oljoro
22
7
7
8
-1
28
9
T/prison
21
4
10
9
-11
26
10
Jkt mgambo
21
7
3
9
-6
24
11
Toto African
24
4
10
1O
-11
22
12
JKT Ruvu
22
6
4
12
-16
22
13
African lyon
23
5
4
14
-19
21
14
Polisi  moro
23
3
10
10
-10
19
MATATIZO YA KIUFUNDI YAKWAMISHA SUPER WEEK ‘LIVE’
Mechi tano kati ya sita za Super Week za Ligi Kuu ya Vodacom zilizokuwa zioneshwe moja kwa moja (live) na Kituo cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini sasa hazitaoneshwa kutokana na matatizo ya kiufundi.
TFF_LOGO12Kwa mujibu wa Mtayarishaji Mtendaji (Executive Producer) wa SuperSport Kanda ya Afrika, Max Tshunungwa ambaye yuko nchini, wameshindwa kuonesha mechi hizo kutokana na matatizo ya kiufundi katika magari yao ya kurushia matangazo (OB van) yanayohudumia Afrika Mashariki- Kenya, Tanzania na Uganda.
Mechi hizo ni kati ya Azam na African Lyon, Yanga na Oljoro JKT, Azam na Simba, Coastal Union na JKT Ruvu na Mgambo Shooting na Yanga itakayochezwa Aprili 17 mwaka huu jijini Tanga.
Tatizo hilo pia limeathiri mechi za Ligi Kuu ya Kenya (KPL) ambazo hazitaonekana wikiendi hii. SuperSport ndiyo yenye haki za matangazo ya televisheni kwa ligi hiyo ya Kenya.
Tshunungwa amekutana na Sekretarieti ya TFF na Kamati ya Ligi kuelezea tatizo hilo. SuperSport kwa kushirikiana na Kamati ya Ligi na TFF watapanga mechi nyingine za Super Week kabla ya ligi kumalizika msimu huu.
Pia TFF, Kamati ya Ligi na SuperSport watakuwa na mkutano mfupi wa waandishi wa habari wakati wa mapumziko kwenye mechi ya leo kati ya Yanga na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)