Friday, April 19, 2013

SIMBA YAPELEKA MKATABA WA NGASA TFF
Club ya Simba SC imeupeleka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mkataba wake mpya na mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa, ambao unaonyesha ataitumikia klabu hiyo na msimu ujao pia, kwa mujibu wa blogu ya bin zubeiry.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya Simba SC, kimesema; “Tumeupeleka mkataba ambao Ngassa alisaini na sisi na TFF wamegonga muhuri wa kuupokea,”.
Kikifafanua, chanzo hicho kimesema; “Sisi tuliununua mkataba wa Ngassa uliokuwa umebaki Azam FC kwa shilingi Milioni 25, kwa hivyo, haki za mchezaji huyo zote zikahamia kwetu,”. “Lakini alipokuja kwetu, tukazungumza naye, akasaini mkataba wa msimu mmoja zaidi kutoka ule mkataba wake uliobaki Azam FC na tulimpa shilingi Milioni 30.

Fedha taslimu Milioni 12 na gari aina ya verosa yenye thamani ya Sh. Milioni 18, akasaini kila sehemu na kuweka dole gumba,”kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, chanzo hicho kimesema kwa sasa Mrisho amekuwa akilalamika kwa uongozi wa Simba kwamba alidhani alipewa Milioni 12 na Verosa ili akubali kuja Simba.
Ikumbukwe awali Ngassa aligoma kupelekwa kwa mkopo Simba SC, hadi alipofanya mazungumzo na viongozi wa klabu hiyo na kufikia makubaliano ndipo akajiunga na klabu hiyo.
Mrisho NgassaLakini chanzo hicho kimesema kwa sasa Mrisho anataka kufanya tena mazungumzo na Simba SC kwa ajili ya kusaini rasmi mkataba mwingine. “Sisi bado tunajiuliza, huyu mtu alikwishasaini na sasa anasema alidhani alipewa fedha na gari ili akubali kuja Simba SC. Inawezekana kwa sababu wachezaji wetu wana  matatizo, wakishaona fedha wao wanasaini tu bila hata kuisoma mikataba,”.

“Bado tunatafakari, tunaweza kurudi naye mezani, ili aitumikie klabu kwa moyo bila kinyongo, au tu tukaamua autumikie mkataba ambao tayari tumekwishausajili na TFF,”kilisema chanzo.
Siku zote, Mrisho mwenyewe amekuwa akisistiza hakusaini mkataba mwingine Simba SC akitokea Azam, bali anajua alikuja kumalizia mkataba wake wa klabu yake ya zamani.

Mrisho Ngassa alipelekwa kwa mkopo Simba baada ya kuonyesha mapenzi kwa klabu yake ya Zamani ya yanga.
IBF YATEUA REFA PAMBANO LA CHEKA VS MASHALI
SHIRIKISHO la Ngumi la Kimataifa (IBF) limeteua refarii na majaji wa pambano la kutetea ubingwa wa Afrika kati ya anayeushukilia ubingwa huo Francis Cheka wa Tanzania na mpinzani wake Thomas Mashali ambaye ni bingwa wa uzito wa Middle ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA). Refarii wa mpambano huo wa kukata na shoka atakuwa ni John Shipanuka kutoka nchini Zambia mbaye alilisimamia pambano kati yaFrancis Chaka na Mada Maugo mwaka jana kwa ustadi mkubwa. Shipanuka ni Afisa Ugavi katika jeshi la Jamhuri ya Watu wa Zambia na ana ujuzi mkubwa wa kusimamia mapambano ya ngumi ya kimataifa.
Aidha, majaji wa mpambano huo ni Daudi Chikwanje kutoka Malawi ambaye ndiye Katibu Mkuu wa Chama Cha Ngumi Cha Malawi na ambaye anakuwa jaji namba moja. Steve Okumu wa Kenya ambaye anakuwa jaji namba mbili na Ismail Sekisambu wa Uganda ambaye anakuwa jaji namba tatu.
Msimamizi mkuu wa mpambano huo ni Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi.Hata hivyo Ngowi amemwagiza Mwenyekiti wa Kamati ya Viwango  na Ushindi wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC)Boniface Wambura amshikie nafasi hiyo ili Ngowi apate nafasi nzuri ya kusimamia mapambano matatu ( moja la ubingwa wa dunia kwa vijana,, lingine la ubingwa wa mabara kwa wanawake na lingine ubingwa wa Afrika) yatakayofanyika nchini Ghana tarehe 3 mwezi Mei.        
Nayo Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini TPBC imeshateua maofisa watakaosimamia mapambano ya awali pamoja na kutoa kibali kwa kampuni ya Mumask Investment and Gebby ili iendeshe mpambano huo"                          
Hii ni mara ya pili kwa bondia Francis Cheka kutetea ubingwa wake tangu amsambaratishe kwa TKO bondia machachari Mada Maugokatika mpambano uliofanyika mwaka jana mwezi wa Aprili katika ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam.
MURRAY ASHINDWA KUSONGA MBELE
MCHEZAJI nyota tetenesi namba moja wa Uingereza, Andy Murray ameshindwa kusonga mbele katika hatua ya nane bora baada ya kukubali kipigo cha 6-1 6-2 kutoka kwa Stanislas Wawrinka katika mzunguko wa tatu wa michuano ya Monte Carlo Masters inayoendelea huko Monaco. Murray ambaye ameshinda mara nane katika mechi 12 walizokutana Wawrinka wa Switzerland katika mchezo huo alionekana kucheza chini ya kiwango chake cha kawaida nafasi ambayo ilitumiwa vyema na mpinzani wake kuhakikisha anaibuka kidedea. Kupoteza mchezo huo ni pigo kubwa kwa Murray ambaye alikuwa akitumia michuano hiyo kujiandaa kwa ajili ya kutetea taji lake la michuano ya wazi ya Ufaransa. Kwa upande mwingine Novak Djokovic na Rafael Nadal wao walifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya kushinda mechi zao.


RAIS wa klabu ya fc Barcelona, Sandro Rosell amebainisha kuwa amepanga kugombea nafasi hiyo kwa kipindi kingine pindi atakapomaliza kipindi cha kwanza mwaka 2016. Rosell alichaguliwa kuwa rais wa klabu hiyo ya Hispania mwaka 2010 ambapo hapo kabla alikuwa mjumbe wa bodi katika uongozi wa aliyekuwa rais wa klabu hiyo Joan Laporta kabla ya kujiuzulu mwaka 2005. Chini ya uongozi wa Rosell Barcelona imefanikiwa kushinda taji moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya, taji lingine moja la Ligi Kuu nchini Hispania na moja la Kombe la Mfalme ambapo msimu huu wako katika nafasi ya kunyakuwa taji lingine la ligi huku wakiwa katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. 
Barcelona inamilikiwa na maelfu ya wanachama ambao huchagua rais na kamati ya utendaji, uchaguzi ambao hufuatiliwa kwa karibu na mashabiki wa soka wa mji huo na nchi nzima kwa ujumla.
BPL: JE NANI KUSHUKA DARAJA, NANI WATANUSURIKA
BPL_LOGO












DONDOO:
Reading na Queens Park Rangers zipo hatarini kushuka daraja .
hata hivyo zipo Aston Villa, Wigan, Stoke City, Sunderland, Norwich na 
Newcastle
MSIMAMO-Timu za chini: kuanzia nafasi ya 8"
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
8
WBA
32
13
5
14
42
43
-1
44
9
SWANSEA
32
10
11
11
43
42
1
41
10
FULHAM
33
10
10
13
44
51
-7
40
11
WEST HAM
33
10
9
14
38
47
-9
39
12
SOUTHAMPTON
33
9
11
13
47
54
-7
38
13
NEWCASTLE
33
10
6
17
42
59
-17
36
14
NORWICH
33
7
14
12
31
52
-21
35
15
SUNDERLAND
33
8
10
15
37
45
-8
34
16
STOKE CITY
33
7
13
13
28
41
-13
34
17
ASTON VILLA
33
8
10
15
36
60
-24
34
18
WIGAN
32
8
7
17
37
58
-21
31
19
QPR
33
4
12
17
29
54
-25
24
20
READING
33
5
9
19
36
63
-27
24
NEWCASTLE UNITED
MECHI ZILIZOBAKI:
Aprili 20: West Brom v Newcastle
April: Newcastle v Liverpool
Mei 4: West Ham v Newcastle.
Mei 12: QPR v Newcastle
May 19: Newcastle v Arsenal




NORWICH CITY
MECHI ZILIZOBAKI:
Aprili 20: Norwich City v Reading
Aprili 27: Stoke v Norwich City
04 Mei 4: Norwich City v Aston Villa
Mei 12: Norwich City v West Brom
Mei 19: Man City v Norwich City







SUNDERLAND
MECHI ZILIZOBAKI:
Aprili 20: Sunderland v Everton
Aprili 29: Aston Villa v Sunderland
06 Mei: Sunderland v Stoke
Mei 12: Sunderland v Southampton
Mei 19: Tottenham v Sunderland





STOKE CITY
MECHI ZILIZOBAKI:
Aprili 20: a v QPR
Aprili 27: Stoke City v Norwich
Mei 6: Sunderland v Stoke City
Mei 12: Stoke City v Tottenham
Mei 19: Southampton v Stoke City






ASTON VILLA
MECHI ZILIZOBAKI:
Aprili 22: Man United v Aston Villa
Aprili 29: Aston Villa v Sunderland
Mei 4: Norwich v Aston Villa
Mei 11: Aston Villa v Chelsea
Mei 19: Wigan v Aston Villa






WIGAN ATHLETIC

MECHI ZILIZOBAKI
Aprili 20: West Ham  v Wigan
Aprili 27: Wigan v Tottenham
Mei 4: West Brom v Wigan
Mei 7: Wigan v Swansea
Mei 11: Wigan v Man City (FA Cup-Fainali, Wembley)
Mei 14: Arsenal v Wigan
Mei 19: Wigan v Aston Villa


QUEENS PARK RANGERS

Aprili 20: QPR v Stoke
Aprili 28: Reading v QPR
Mei 4: QPR v Arsenal
Mei 12: QPR v Newcastle
Mei 19: Liverpool v QPR




READING
Aprili 20: Norwich v Reading
Aprili 28: Reading v QPR
Mei 4: Fulham v Reading
Mei 12: Reading v Man City
Mei 19: West Ham v Reading
Neil Warnock says:





MSIMAMO==BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE 
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
MAN UNITED
33
26
3
4
75
35
40
81
2
MAN CITY
32
20
8
4
58
27
31
68
3
CHELSEA
32
18
7
7
64
33
31
61
4
ARSENAL
33
17
9
7
64
35
29
60
5
TOTTENHAM
32
17
7
8
55
40
15
58
6
EVERTON
33
14
14
5
51
37
14
56
7
LIVERPOOL
33
13
11
9
59
40
19
50










SITA WAUMANA KUWANIA TUZO YA PFA MCHEZAJI BORA"








WAGOMBEA TUZO HAWA PFA" BORA'
Michael Carrick (Manchester United)
Gareth Bale (Tottenham Hotspur)
Robin van Persie (Manchester United
Luis Suarez (Liverpool)
Eden Hazard (Chelsea)
Juan Mata (Chelsea)
WASHINDI WA PFA WALIOPITA:
2011-12: Robin van Persie (Arsenal)
2010-11: Gareth Bale (Spurs)
2009-10: Wayne Rooney (Man Utd)
2008-09: Ryan Giggs (Man Utd)
2007-08: C Ronaldo (Man Utd)
2006-07: C Ronaldo (Man Utd)
LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KUANZA MEI 12

Ligi ya Mabingwa wa Mikoa kutafuta timu tatu zitakazopanda kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao chini ya usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itaanza Mei 12 mwaka huu.
Mwisho wa mikoa kuwasilisha majina ya mabingwa wao ni Mei 1 mwaka huu wakati ratiba ya ligi hiyo itapangwa mbele ya waandishi wa habari Mei 3 mwaka huu kwenye ofisi za TFF.
Uwasilishaji wa jina la bingwa wa mkoa unatakiwa kufanyika pamoja na ulipaji ada ya ushiriki ambayo ni sh. 100,000. Mfumo wa ligi hiyo ni bingwa wa mkoa X kucheza na bingwa wa mkoa Y nyumbani na ugenini ambapo mshindi ndiye anayesonga mbele katika hatua inayofuata.
Usajili wa wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika hatua ya mkoa na unatakiwa kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho. TFF inapenda kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya ligi hiyo.
KILA LA KHERI AZAM FC
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri timu ya Azam FC katika mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco itakayochezwa kesho (Aprili 20 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Azam FC ina fursa nzuri ya kufanya vizuri kwenye mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Emile Fred kutoka Shelisheli kutokana na maandalizi iliyofanya, lakini vilevile tunatoa mwito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuiunga mkono.
Makocha wasaidizi wa timu zote mbili, Kalimangonga Ongala wa Azam na Lahcen Ouadani wa AS FAR Rabat wamezungumza na waandishi wa habari kuhusu mechi hiyo, kuwa wamejiandaa kuibuka na ushindi.
Kocha Ongala amesema wamepata DVD za mechi tatu za mwisho za AS FAR Rabat, moja ikiwa dhidi ya timu ya Al Nasir ya Libya ambayo waliitoa katika raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho na nyingine mbili za ligi ya Morocco ambazo wanazifanyia kazi kuhakikisha wanashinda kesho.
Naye Ouadani amesema hawaifahamu vizuri Azam, lakini wanaujua mpira wa Tanzania baada ya kuangalia mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco (Lions of the Atlas) iliyochezwa jijini Dar es Salaam Machi 24 mwaka huu na Stars kushinda mabao 3-1.
Baadhi ya wachezaji ambao Azam inatarajia kuwatumia kwenye mechi ya kesho ni pamoja na Aishi Manula, Mwadini Ally, Khamis Mcha, John Bocco na Salum Abubakar ambao pia wamo kwenye kikosi cha sasa cha Taifa Stars kilicho chini ya kocha Kim Poulsen.
AS FAR Rabat ina wachezaji sita kwenye timu ya Taifa ya Morocco. Wachezaji hao ni mabeki Younes Bellakhdar, Abderrahim Achchakir, Younnes Hammal, na viungo Salaheddine Said, Salaheddine Aqqal na Youssef Kaddioui.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)