Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Ruvu Shooting na Simba iliyokuwa ichezwe leo (Aprili 25 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sasa itafanyika Mei 5 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
Mabadiliko hayo yametokana na Serikali kuutumia uwanja kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Muungano ambazo kitaifa zitafanyika kesho (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaomba radhi washabiki kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo na ghafla. Ratiba ya mechi nyingine za VPL zinabaki kama zilivyo.
Ligi hiyo inaendelea kesho (Aprili 26 mwaka huu) kwa mechi kati ya Coastal Union na Azam itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Jumapili (Aprili 28 mwaka huu) itakuwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni Simba dhidi ya Polisi Morogoro.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
OLIVER USO KWA USO NA FA
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Oliver Giroud amekishambulia Chama cha Soka nchini Uingereza-FA baada ya uamuzi wake wa kutupilia rufani yake ya kupinga kadi nyekundu aliyopewa. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alitolewa nje na mwamuzi Andre Marriner kwa kumchezea vibaya Stanislav Manolev wakati wa mchezo baina ya Arsenal na Fulham Jumamosi iliyopita hivyo kupelekea kufungiwa mechi tatu kwasababu ya kupewa kadi nyekundu ya moja kwa moja. Giroud mwenye umri wa miaka 26 amekuwa akijitetea kwamba aliteleza bahati mbaya kwenye tukio hilo na baada ya rufani yake kutupiliwa mbali amewakosoa FA kwa hatua waliyochukua. Giroud amesema ameshangazwa na hatua iliyochukuliwa na FA dhidi yake, sio kwamba imemuumiza ila anadhabu sheria za Uingereza zimekuwa kali sana ukilingasha na makosa yanayofanywa.