Friday, April 26, 2013

RUVU SHOOTING, SIMBA SASA KUCHEZA MEI 5
Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Ruvu Shooting na Simba iliyokuwa ichezwe leo (Aprili 25 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sasa itafanyika Mei 5 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.

Mabadiliko hayo yametokana na Serikali kuutumia uwanja kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Muungano ambazo kitaifa zitafanyika kesho (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawaomba radhi washabiki kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo na ghafla. Ratiba ya mechi nyingine za VPL zinabaki kama zilivyo.

Ligi hiyo inaendelea kesho (Aprili 26 mwaka huu) kwa mechi kati ya Coastal Union na Azam itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Jumapili (Aprili 28 mwaka huu) itakuwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni Simba dhidi ya Polisi Morogoro.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

OLIVER USO KWA USO NA FA
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Oliver Giroud amekishambulia Chama cha Soka nchini Uingereza-FA baada ya uamuzi wake wa kutupilia rufani yake ya kupinga kadi nyekundu aliyopewa. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alitolewa nje na mwamuzi Andre Marriner kwa kumchezea vibaya Stanislav Manolev wakati wa mchezo baina ya Arsenal na Fulham Jumamosi iliyopita hivyo kupelekea kufungiwa mechi tatu kwasababu ya kupewa kadi nyekundu ya moja kwa moja. Giroud mwenye umri wa miaka 26 amekuwa akijitetea kwamba aliteleza bahati mbaya kwenye tukio hilo na baada ya rufani yake kutupiliwa mbali amewakosoa FA kwa hatua waliyochukua. Giroud amesema ameshangazwa na hatua iliyochukuliwa na FA dhidi yake, sio kwamba imemuumiza ila anadhabu sheria za Uingereza zimekuwa kali sana ukilingasha na makosa yanayofanywa.

Thursday, April 25, 2013

TIMU ZA HISPAIN HOI BUNDASLIGA NOMA KWELI KWELI"TAZAMA MAMBO YALIVYOKUWA"

Katika mechi ya usiku  huu mchezaji aliye katika kiwango bora kabisa Robert Lewandowski  yameipa Borussia Dortmund ushindi wa 4-1 dhidi ya Real Madrid katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya nchini Ujerumani.
Mabao ya mshambuliaji huyo wa Poland yameipa  Dortmund kujiweka katika nafasi nzuri ya kutingaa fainali ya klabu za bundasliga pekee  itakayopigwa Uwanja wa Wembley mwezi ujao, kufuatia jana Bayern Munich kuichapa 4-0 Barcelona nchini Ujerumani pia.
Lewandowski alifunga bao la kwanza dakika ya nane, kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia Real dakika ya 43.
Lakini lewandowski akaonyesha makali yake katika kipindi cha pili na kufunga mabao matatu zaidi dakika za 50, 55 na 67 kwa penalti.
Kocha wa Real, Mreno Jose Mourinho ambaye hakutegemea kipigo hicho kitakatifu, sasa real madrid inatakiwa  kutengeneza mipango ya kushinda 3-0 katika mchezo wa marudiano wiki ijayo, ili kuwapiku Dortmund.




UCL-NUSU FAINALI
RATIBA:
MARUDIANO
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumanne Aprili 30
Real Madrid v Borussia Dortmund [1-4]
Jumatano Mei 1
Barcelona v Bayern Munich [0-4]
FAINALI
25 Mei 2013

UWANJA wa WEMBLEY, London.

Wednesday, April 24, 2013

TAFAKARI YA LEO 
TOMATH MULLER 
Taarifa kamili
Jina kamili”
Thomas Müller
Kuzaliwa”
13 September 1989 (age 23)
Mahali”
Weilheim, West Germany
Urefu”
1.86 m (6 ft 1 in)
Nafasi anayocheza”
Timu ya sasa
Current club
Number
25
Timu za vijana*
1993–2000
TSV Pähl
2000–2008
Timu ya Ukubwa*
Years
Team
Mechi
(Goli)
2008–2009
35
(16)
2008–sasa
131
(44)
Timu ya Taifa
2004–2005
6
(4)
2007
1
(0)
2008
1
(1)
2009–2010
6
(1)
2010–
41
(13)
AJIWEKA PEMBENI KAMATI YA FIFA
MJUMBE wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Nicolas Leoz kutoka Paraguay amejiuzulu wadhifa wake huo kutokana na kile alichodai kuwa na matatizo ya kiafya ikiwa ni siku chache kabla ya shirikisho hilo halijatangaza uchunguzi wa bakshishi katika michuano ya Kombe la Dunia. FIFA ilithibitisha kupokea barua ya Leoz mwenye umri wa miaka 84 ambaye pia ataachia ngazi wadhifa wake wa urais wa Shirikisho la Soka la Amerika Kusini-CONMEBOL. Leoz ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo mara kadhaa amekuwa mjumbe katika bodi ya FIFA kuanzia mwaka 1998 na amekuwa rais wa CONMEBOL kuanzia mwaka 1986. Katika barua yake Leoz amesisitiza kuwa uamuzi aliochukua ni binafsi kutokana na matatizo ya kiafya aliyonayo kwani hawezi kusafiri mara tano kwa mwaka kama ilivyokuwa zamani.


Ijapo kuwa matajiri wa london Man city wameonekana kuvutiwa na kiwango chake KLABU ya Paris Saint-Germain-PSG ya Ufaransa imemtengea mkataba mnono wa euro milioni 8.5 kwa msimu mshambuliaji nyota wa Napoli ya Italia Edinson Cavani. Imeripotiwa na vyombo vua habari nchini humo kuwa mkurugenzi wa michezo wa klabu ya PSG, Leonardo ameshafanya vikao kadhaa na wakala wa nyota huyo kuzungumzia uhamisho wake kutoka Napoli ambao unakaribia kufikia kiasi cha euro milioni 63. Mbali na PSG vilabu vingine vikubwa barani Ulaya ambavyo vimeonyesha nia ya kuhitaji sahihi ya nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay ni pamoja na Real Madrid, Manchester City na Chelsea. Cavani mwenye umri wa miaka 26 ana mkataba na Napoli mpaka 2015 ambao unamuwezesha kulipwa kiasi cha euro milioni 1.4 kwa msimu.
MKALI RONALDINHO APEWA UNAHODHA VS CHILE:;
RONALDINHO anatarajiwa kupewa unahodha wa timu ya taifa ya Brazil katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Chile hatua ambayo itamuweka katika nafasi nzuri ya kujumuishwa katika kikosi kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho.
Kocha wa Brazil Luis Felipe Scolari ameonyesha matumaini yake kwa Ronaldinho ambaye amaewahi kunyakuwa tuzo ya mchzaji bora wa dunia mara mbili kwa kumpa unahodha kwenye mechi ya mwisho kabla hajatangaza kikosi cha michuano ya Kombe la Shirikisho.
Scolari tayari amebainisha kuwa kuna uwezekano akamchukua kati ya Ronaldinho au Kaka kwa ajili ya michuano hiyo itakayofanyika June mwaka huu. Kaka atakosa mchezo dhidi ya Chile kwasababu ni wachezaji wanaocheza katika vilabu vya Brazil peke ndio waliochaguliwa kwa ajili ya mchezo huo kirafiki kitendo ambacho kinampa nafasi kubwa kama akionyesha kiwango kizuri.
MUNICH YAITANDIKA BARCA 4-MTUNGI ANGALI MAMBO YA JANA
MABINGWA wa Ujerumani maarufu BUNDASLIGA, Bayern Munich wamejiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuitandika Barcelona 4-0 katika mchezo wa kwanzawa nusu fainali nchini Ujerumani. Mabao mawili ya Thomas Müller, na yale ya Mario Gomez na Arjen Robben yaliizamisha Barcelona ambayo ilikuwa na nyota wake wote wakutegemewa, akiwemo Messi ambaye alikosa michezo kadhaa kabla ya kuanzishwa usiku huu. Hii imekuwa mara ya kwanza kwa Barcelona kufungwa mabao 4-0 tangu mwaka 1997 walipofungwa na Dynamo Kiev ya Urusi mwaka 1997 kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya. Bayern Munich wametoka kutawazwa kuwa mabingwa wa Ujerumani wiki chache zilizopita na iwapo watafanikiwa kuiondosha Barcelona na kutinga hatua ya fainali ya michuano ya klabu bingwa, itakuwa fainali yao ya tatu kushiriki ndani ya miaka minne. Michuano hiyo itaendelea tena leo usiku ambapo mahasimu wa Barcelona, Real Madrid watakuwa na kibarua kizito pale itakapokaribishwa katika Uwanja wa Signal-Iduna-Park kukwaana na wenyeji Borussia Dortmund kwenye mchezo unaotaajiwa kuwa mgumu na wa kusisimua.
TAIFA STARS KUCHEZA MICHUANO YA COSAFA

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itashiriki michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) itakayofanyika Julai mwaka huu nchini Zambia. Taifa Stars inashiriki michuano hiyo ya timu za Taifa za nchi wanachama wa COSAFA ikiwa timu mwalikwa. Nchi wanachama wa COSAFA ni Afrika Kusini, Angola, Botswana, Comoro, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Swaziland, Zambia na Zimbabwe. Michuano hiyo itafanyika kuanzia Julai 6 hadi 21 mwaka huu katika miji ya Lusaka, Ndola na Kabwe. Ratiba ya makundi ya michuano hiyo itapangwa Mei 3 mwaka huu jijini Lusaka. Mara ya mwisho michuano hiyo ilifanyika miaka mitatu iliyopita. Hii itakuwa mara ya pili kwa Tanzania kushiriki michuano hiyo baada ya kucheza ya kwanza iliyofanyika mwaka 1996 nchini Zimbabwe. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inatarajia kuingia kambini mwishoni mwa mwezi ujao kujiandaa kwa mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech. Juni 16 mwaka huu Taifa Stars itacheza na Ivory Coast jijini Dar es Salaam katika mechi nyingine ya mchujo ya Kombe la Dunia wakati Juni mwishoni na Julai mwanzoni itacheza mechi ya Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) dhidi ya Uganda. Wakati huo huo, waandishi wa habari wanaotaka kuripoti michuano hiyo wanatakiwa kuwasilisha majina yao TFF kabla ya Aprili 27 mwaka huu ili maombi yao yatumwe COSAFA kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho (Accreditation).