Mabingwa wa kandanda katika jiji la londond Manchester United na Real Madrid,zinataraji kukutana katika dimba la Uwanja Old Trafford Juni 2 kucheza Mechi maalum itakayoshirikisha Manguli wa Klabu hizo ili kusaidia Mfuko wa Hisani wa Klabu ya Manchester United uitwao RED HEART UNITED.
Mechi hiyo inafuatia ile iliyochezwa Tarehe 3 Juni 2012 huko Santiago Bernabeu kati ya Timu hizi iliyochezwa na Mastaa wa zamani wa Timu hizi ili kutunisha Mfuko wa Hisani wa Real Madrid.
Kwenye Mechi itakayochezwa Juni 2 Uwanjani Old Trafford, kutakuwa na utangulizi wa Shoo Laivu ya Muziki itakayoshirikisha JLS na Amelia Lily.
Kikosi cha Man United kitakuwa chini ya Meneja Bryan Robson ambae aliwahi kuwa Nahodha wa Man United na watawania kulipa kisasi cha kufungwa 3-2 huko Madrid Mwaka jana na safari hii kimeongezwa nguvu kwa kuwepo Mabeki imara toka Norway Ronny Johnsen na Henning Berg ambao walitamba sana Old Trafford enzi zao.
Pia Wachezaji wengine wataongezeka
Man United: Edwin van der Sar, Raimond van der Gouw; Clayton Blackmore, Denis Irwin, Jaap Stam, Lee Martin, Ronny Johnsen, Henning Berg; Jesper Blomqvist, Lee Sharpe, Quinton Fortune; Andy Cole, Dion Dublin, Teddy Sheringham, Dwight Yorke.
Real Madrid: Pedro Contreras; Fernando Hierro, Ivan Helguera, Manolo Sanchis, Christian Karembeu; Claude Makelele, Zinedine Zidane, Steve McManaman, Fernando Redondo, Luis Figo, Guti, Jose Amavisca; Ruud van Nistelrooy, Emilio Butragueno, Alfonso Perez.
USO KWQA USO 3 JUNI 2012:
REAL MADRID 3 MAN UNITED 2
Santiago Bernabeu Stadium
Watazamaji: 65,000
MAGOLI:
Real Madrid:
-Morientes
-Figo
-Redondo
Manchester United
-Lee Sharpe
-Teddy Sheringham
VIKOSI:
Real Madrid: Buyo, Chendo, Roberto Carlos, Hierro, Sanchis, Zidane, Redondo, Butragueño, Morientes, Martin Vazquez, Figo
Man United: Van der Sar, Lee Martin, Irwin, Fortune, Johnsen, Dublin, Cole, Sheringham, Lee Sharpe, Blomqvist, Yorke