Friday, April 26, 2013

MBOMA AWANIA UKOCHA TUIMU YA TAIFA CAMAROON
Ancien du PSG Aristide Arthode Deuhla-Patrick Mboma.JPGCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Cameroon, Patrick Mboma ameonyesha nia yake ya kuifundisha timu ya taifa ya nchi hiyo na anakusudia kutuma maombi yake Shirikisho la Soka la Cameroon-Fecafoot siku moja baada ya Waziri wa Michezo Adoum Garoua kulitaka shirikisho hilo kufanya mchakato wa kupata kocha mpya. Mshambuliaji huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 42 alikuwemo katika kikosi cha nchi hiyo ambacho kilinyakuwa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2000 na 2002 na pia kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika. Hata hivyo Mboma hajawahi kufundisha timu yoyote na wadau wa soka nchini humo wamedai kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Paris Saint Germain na Parma hana uzoefu wa kutosha wa kumuwezesha kupewa nafasi ya kuinoa timu hiyo. Lakini pamoja na wadau kuponda uwezo wake Mboma amesema haimkatishi tamaa na atatuma maombi yake kuiwinda nafasi hiyo.

Kuhusu yeye
Full nameHenri Patrick M'Boma Dem
Date of birthNovember 15, 1970 (age 42)
Place of birthDoualaCameroon
Height1.85 m (6 ft 1 in)
Playing positionStriker
Timu alizocheza
YearsTeamApps(Gls)
1990–1992Paris Saint-Germain0(0)
1992–1994Châteauroux48(22)
1994–1995Paris Saint-Germain8(1)
1995–1996Metz17(4)
1996–1997Paris Saint-Germain8(1)
1997–1998Gamba Osaka34(29)
1998–2000Cagliari40(15)
2000–2001Parma24(5)
2002→ Sunderland (mkopo)9(1)
2002–2003Al-Ittihad28(12)
2003–2004Tokyo Verdy 196935(17)
2004–2005Vissel Kobe10(2)
Total261(109)
Timu ya taifa"
1995–2004Cameroon57(33)
TUZO-AWARDS
3.African Nations Cup top scorer: 2002
Cameroon national team
YearAppsGoals
199510
199611
1997106
199881
199943
200099
200194
2002105
200310
200444
Total5733

[edit]