Friday, June 21, 2013

NANI ZAIDI KESHO RED'S MISS TANGA 2013 MKWAKWANI.

Kesho ndio Kesho  Juni 22,2013 Katika Uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga utakutanisha walimbwende washindano la Miss Tanga 2013 litakalo fanyika katika uwanja huu.
Wakizungumza na mkali wa dimba mkaoni hapa baadhi ya walimbwende hao wamesema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanakonga Nyoyo za wadau mbalimbali  watakao jitokeza katika kushuhudia mvutano huo.
Aidha mamiss hao walikuwa katika ziara ya Makamu wa Rais, Dk Mohammed Ghalib Bilal kuzindua mradi wa uwekezaji wa viwanda katika eneo pongwe jijini hapamapema leo asubuhi.  Katika uzinduzi huo awali Rais Dk. Jakaya Kikwete ndiye aliyetarajiwa kuja kuzindua mradi huo, lakini badala yake amekuja Dk Bilal. 
Hivyo katika shindano hilo mshindi wa kwanza anatarajiwa kujinyakulia kitita cha sh.laki tano 500,000 huku msanii wa muziki wa kizazi kipya, Tunda Man, akiongoza kwa upande wa Burudani, katika shindano litakalofanyika Jumamosi katika uwanja wa Mkwakwani.
Akizungumza na mkali wa dimba jijini hapa Mkurugenzi wa Kampuni ya DATK Intertainment Asha Kigundula,amesema kuwa maandalizi ya shindano hilo yapo vizuri kwa asilimia 100% ambapo zawadi kwa mshindi wa pili atajinyakulia kitita cha shilingi 300,000.
Mshindi wa tatu atazawadiwa kitita cha shilingi  250, 000 wakati mshindi wa nne na tano wakipata sh.200, 000 kila mmoja na warembo wengine watakaosalia watapata kitita cha sh.laki moja moja kila mmoja 100,000 kama kifuta jasho pamoja na zawadi kwa mrembo mwenye nidhamu ili kuweza kuboresha shindano hilo.
Kwa upande wa Burudani msanii wa kizazi kipya, Tunda Man, ataongoza safu ya burudani, ambapo itakuwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Dr John, Nabisha kutoka kundi la THT, Fady Dady na wasanii chipukizi kutoka mkoani hapa.

Warembo hao ni Hawa Ramadhani (18),Hazina Mbaga (19)Like Abdulraman (19), Irene Thomas(20), Tatu Athumani (19), Winfrida Gutram (21)Lulu Mbonela (19) ,Hazina Daniel (19),Lulu Matawalo(22),Judithi Moleli (21),Neema Jonas na Hawa Twaybu(21)

Wakati huo huo Warembo hao wanaowania Taji la Mlimbwende wameiomba Halmashuri ya Jiji la Tanga kuifanyia marekebisho barabara inayokwenda katika mapango ya Amboni ili iweza kuwa nzuri na ipitike kirahisi nyakati zote.

MIAMI HEAT YATWAA TAJI LA PILI LIGI YA NBA-MAREKANI"

 TIMU ya mpira wa kikapu Miami Heat imefanikiwa kutwaa taji la pili mfululizo la Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani-NBA baada ya kuibamiza timu ya San Antonio Spurs kwa vikapu 95-88 katika fainali ya saba iliyofanyika katika Uwanja wa American Airlines uliopo jijini Miami, Florida. San Antonio walibakiza kidogo kulinyakuwa taji hilo Jumanne kabla ya Miami kupambana na kushinda hivyo kuzifanya timu hizo kutoka sare ya kufunga 3-3 katika fainali ya sita kati ya saba ambazo wanatakiwa kucheza. 
Katika mchezo wa Alfajiri kuamkia leo nyota wa timu ya Heat, LeBron James mwenye umri wa miaka 28 alifanikiwa kuisadia vyema timu yake kwa kufunga vikapu 37 na kutajwa kuwa mchezaji mwenye thamani zaidi katika ligi hiyo kwa mara ya pili mfululizo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo James ambaye aliingia matatani baada ya kudaiwa kucheza chini ya kiwango katika mechi muhimu amesema anajisikia fahari kunyakuwa taji hilo katika uwanja wao wa nyumbani na yote yaliyopita yanabaki kuwa historia.

WANANDINGA WA HISPAIN WAPORWA HOTELI-BRAZIL

Katika taarifa iliyoripotiwa na vyombo vya habari nchini Hispania vimeripoti kuwa wachezaji sita wa timu ya taifa ya Hispania wameibiwa fedha zao katika vyumba walivyofikia katika hoteli moja jijini Recife wakati wanacheza mchezo wao ufunguzi wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Uruguay. Mojawapo ya wachezaji waliokumbwa na zahama hilo ni beki wa Barcelona, Gerard Pique ambaye aligundua kaibiwa wakati aliporejea chumbani kwake baada ya mchezo dhidi ya Uruguay ambao walishinda kwa mabao 2-1. Msemaji wa Shirikisho la Soka Dunia-FIFA, Pekka Odriozola alikiri kupata taarifa hizo lakini wameziachia mamlaka husika kushughulikia na kisha kuwaletea taarifa kamili. Hispania ambao wako kundi B jana wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwa ushindi mkubwa baada ya kuitandika Tahiti kwa mabao 10-0 wakati wawakilishi pekee wa Afrika kwenye mashindano hayo walishindwa kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Uruguay.

Thursday, June 20, 2013

BRAZIL YAFANYA KWELI KOMBE LA MABARA-

TIMU ya taifa ya Brazil imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi yake ya pili ya Kombe la Mabara ambapo mshambuliaji mpya wa FC Barcelona Neymar akiifungia  timu yake bao  safi kunako dakika ya 10 ya kipindi cha kwanza kabla ya kumtengenezea nafasi ya kufunga bao la pili Jo.
Brazil imeichalaza Mexico mabao 2-0 ambapo sasa imefanikiwa kufikisha ponti sita na kuzidi kuziweka katika nafasi nzuri na kuongoza Kundi A.
katika goli hili hilo Daniel Alves alipiga krosi  safi kutoka kulia ambapo ilimfikia Neymar akaitokea kwa mbele ya beki wa Mexico, kabla ya kuhadaa na kumtungua kipa Jose Corona dakika ya tisa na dakika ya 90 akampa pande Jo kufunga la pili.
Katika mchezo huo uliokuwa chini refa Howard Webb wa Uingereza, kikosi cha Brazil kilikuwa: Cesar, Alves, Silva, Luiz, Marcelo, Luiz Gustavo, Paulinho, Oscar/Hernanes dk62, Hulk/Lucas Moura dk78, Neymar na Fred. 
Mexico: Corona, Rodriguez, Salcido,  Torrado, Dos Santos, Henandez, Moreno,  Guardado, Torres/Barrera dk70, Mier na Flores/Herrera dk68.
MSIMAMO KUNDI A
NA
TIMU
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Brazil
2
 2
0
0
  5
 0
  5
 6
2
Italy
2
 2
0
0
  6
 4
  2
 6
3
Mexico
2
 0
0
2
 1
 4
 -3
 0
4
Japan
2
 0
0
2
 3
  7
 -4
 0
MSIMAMO KUNDI B
NA
TIMU
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Nigeria
1
 1
0
0
 6
 1
 5
 3
2
Hispain
1
 1
0
0
 2
 1
 1
 3
3
Uruguay
1
 0
0
1
 1
 2
-1
 0
4
Tahiti
1
 0
0
1
 1
 6
 -5
 0
RATIBA LEO 
Alhamis Juni 20
Saa 4 usiku
Spain vs Tahiti
 Saa 7 usiku
Nigeria vs Uruguay 

TAFAKARI YA LEO NA EDEN HAZARD KATIKA HARAKATI ZA ULIMWENGU WA SOKA.

TAARIFA KUHUSU YEYE
Full nameEden Hazard
Date of birth7 January 1991 (age 22)
Place of birthLa Louvière, Belgium
Height1.70 m (5 ft 7 in)
Playing positionWinger
TAARIFA KUHUSU CLUB
Timu ya sasaChelsea
Number17
TIMU ZA UJANA
1995–2003Royal Stade Brainois
2003–2005Tubize
2005–2007Lille
TIMU ZA UJANA
MwakaTimuMechiGoli
2007–2012Lille147(36)
2012–Chelsea34(9)
TIMU YA TAIFA
2006Belgium U155(1)
2006Belgium U164(2)
2006–2008Belgium U1717(2)
2007–2009Belgium U1911(6)
2008–Belgium37(5)

TUZO NA VILABU
Lille fc
Ligue 1 (1): 2010-11
Coupe de France (1): 2010-11
Chelsea 
UEFA Europa Ligi (1): 2012-13
TUZO BINAFSI
UNFP Ligue 1 Mchezaji wa Mwaka (2): 2010-11, 2011-12
UNFP Ligue 1 Mchezaji  kijana wa Mwaka (2): 2008-09, 2009-10
UNFP Ligue 1 Timu ya Mwaka (3): 2009-10, 2010-11, 2011-12
UNFP Mchezaji wa Mwezi (3): Machi 2010, Machi 2011, [221] Machi 2012
Ligi Kuu ya PFA Timu ya Mwaka (1): 2012-13
Bravo tuzo (1): 2011 

SERENA WILLIAMS AOMBA RADHI KATIKA GAZETI"

Mwanariadha nyota wa kike mahiri katika mchezo wa tenisi anayeshika namba moja katika orodha za ubora duniani kwa upande wanawake, Serena Williams ameomba radhi kwa kauli aliyoitoa katika gazeti la Rolling Stone kuhusiana na kesi ya ubakaji. Nyota huyo ambaye anatarajiwa kutetea ubingwa wake wa michuano ya Wimbledon alikaririwa na gezeti kuhusiana na kesi hiyo inayoendelea katika mji wa Steubenville, Ohio, Marekani. Katika kesi hiyo wachezaji wawili wa mpira wa miguu wa kimarekani wanatuhumiwa kumbaka msichana aliyelewa mwenye umri wa miaka 16 tukio ambalo walilifanya Machi mwaka huu. Gazeti hilo la Rolling Stone lilimkariri Williams akidai kuwa hamlaumu msichana huyo lakini kama una umri wa miaka 16 na unakunywa kiasi hicho wazazi wako wanatakiwa kukufundisha kwamba usipokee kinywaji kutoka kwa mtu usiyemfahamu.Kauli yake hilo ilishambuliwa na watu mbalimbali nchini humo mpaka kupelekea nyota kuomba radhi akidai kuwa hakumaanisha kama watu wanavyofikiri.

ANZHI MAKHACHKALA KUFUNGIWA NA UEFA.

Timu ya soka ya Anzhi Makhachkala ya Urusi kwa mara nyingine haitacheza mechi zake za Europa League msimu ujao mbali na uwanja wao wa nyumbani baada ya kufungiwa na Shirikisho la Soka barani-UEFA humo kwasababu za kiusalama. Katika taarifa ya UEFA iliyotumwa katika mtandao wake imedai kuwa baada ya kufanya utafiti wa usalama katika mji wa Kaskazini wa Caucasus ambao klabu hiyo inatoka wamegundua kuwepo usalama mdogo hivyo hawatoruhusu timu hiyo kucheza mechi zake nyumbani. UEFA imeitaka klabu hiyo kutafuta uwanja mbadala kwa ajili ya mechi zake za nyumbani za Europa League msimu wa 2013-2014. Anzhi walimaliza katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Urusi msimu uliopita na kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.