Katika msimu uliopita, kulikuwa na wafungaji kadhaa ambao walitikisa, lakini nyota wa Hispania katika ligi ya BBVA LA LIGA ndio walionyesha umahiri zaidi.
Wafuatano ni nyota watano ambao ndiyo wakali wa kutikisa nyavu Ulaya. Nyota watatu kati yao ni kutoka Ligi Kuu Hispania.
1. Lionel Messi (Barcelona)
Mabao 46 katika mechi 32 za ligi. Huyu ameonyesha uwezo na umwamba mkubwa kwa kuwapita wachezaji wengine wa Ulaya kwa mabao zaidi ya 12.
2. Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
2. Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
Amefunga jumla ya mabao 146 kwenye mechi 135 za ligi tangu alipotua kwenye kikosi cha Real Madrid mwaka 2009.
hivyo kila mtu anafahamu kabisa kuwa Ronald ndie mpinzani mkuu wa messi ambapo tokea alipotua Madrid ameonyesha upinzani mkubwa kwa messi lakini bado alionekana kuwa nyuma ya messi katika kutupia mabao.
3. Radamel Falcao (Atletico Madrid)
Mabao 28 katika mechi 33 za ligi. Nyota huyo raia wa Colombia, ameisaidia timu yake kushika nafasi ya tatu msimu huu.Hakufanya vizuri kwenye ligi kuu pekee, bali pia kwenye mechi za Super Cup na Europa League ambapo alifunga mabao sita kwenye michuano hiyo mikubwa .Ni mmoja kati ya wachezaji wanaosakwa mno. Chelsea ndio klabu inayomwania kwa karibu kwa kuwa Jose Mourinho amerudi Stamford, huenda akamnasa kirahisi.
4. Edinson Cavani (Napoli)
Mabao 28 katika mechi 33 za ligi. Mbinu, kasi, maarifa na nguvu ndio mambo yanayomfanya nyota huyo asakwe na klabu kubwa za Ulaya msimu huu.
Huenda akasajiliwa na Man City au Chelsea kwani ndio timu zilizo mstari wa mbele kuwania saini yake.Hata hivyo Napoli imesema kuwa haiwezi kumuuza kwa chini ya Pauni 50 milioni.
5. Zlatan Ibrahimovic (PSG)
