Thursday, July 25, 2013
RODGERS ADAI OFA WALITOA ARSENAL HAILINGANI NA THAMANI YA MCHEZAJI HUYO
JAVU ASAINI JANGWANI KUIMARISHA SAFU YA USHAMBULIAJI YA YANGA
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga SC, Abdallah Bin Kleb amesema kwamba wamemalizana na Javu pamoja na klabu yake, Mtibwa na sasa huyo ni mchezaji mpya wa Jangwani.
TAIFA STARS YATUA UGANDA KUIVAA THE CRANES

Stars ambayo iliwasili ikitokea jijini
Mwanza ilipokuwa imepiga kambi ya siku kumi kujiandaa kwa mechi hiyo
itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itakwenda Afrika Kusini
mwakani imefikia hoteli ya Mt. Zion iliyoko eneo la Kisseka katikati ya
Jiji la Kampala.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars inayodhaminiwa
na Kilimanjaro Premium Lager, Kim Poulsen ameridhishwa na kiwango cha
hoteli hiyo, kwani ndiyo ambayo timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro
Stars) ilifikia Novemba mwaka jana ilipokuja Kampala kushiriki michuano
ya Kombe la Chalenji inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu
Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Stars ambayo ilitiwa chachu na Rais
Jakaya Kikwete alipokutana nayo Uwanja wa Ndege wa Mwanza wakati
ikiondoka kuja Kampala, na kuitakia kila la kheri itafanya mazoezi yake
ya mwisho kesho (Julai 26 mwaka huu) Uwanja wa Mandela kujiandaa kwa
mechi ya Jumamosi.
Kocha Kim amesema ingawa mechi hiyo ni
ngumu, lakini kikosi chake kimejiandaa kuikabili Uganda kwani wachezaji
wako wako vizuri na ari kwa ajili ya mechi iko juu.
Wachezaji wote wako katika hali nzuri,
isipokuwa Khamis Mcha aliyekuwa na maumivu ya goti, lakini kwa mujibu wa
madaktari wa timu anaendelea vizuri kwani tayari wanampa mazoezi
mepesi.
Kikosi cha kamili cha Stars ilichoko
hapa kinaundwa na makipa Juma Kaseja, Mwadini Ali na Ali Mustafa. Mabeki
ni Aggrey Morris, David Luhende, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Nadir
Haroub na Vincent Barnabas.
Viungo ni Amri Kiemba, Athuman Idd,
Frank Domayo, Haruni Chanongo, Khamis Mcha, Mudhathir Yahya, Salum
Abubakar na Simon Msuva. Washambuliaji ni John Boko, Juma Luizio na
Mrisho Ngasa.
Wakati huo huo, Kocha Kim Poulsen
atakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari siku ya Jumatatu (Julai 29
mwaka huu). Mkutano huo utafanyika saa 5 kamili asubuhi katika ukumbi wa
mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Tuesday, July 23, 2013
FC BARCA YATARAJI KUMTANGAZA MARTINO KUWA KOCHA MPYA
Gerardo Martino ambaye ni raia wa Argentina,Kocha wa Newell’s Old Boys ya huko Argentina, anatarajiwa kutangazwa
kuwa Kocha mpya wa FC Barcelona kuchukua nafasi iliyoachwa wazi Tito Vilanova kutokana na sababu za kiafya.
Martino, mwenye Miaka 50, anategemewa kusaini Mkataba wa Miaka mitatu na kutangazwa rasmi baadae Wiki hii.
JINA: Gerardo Daniel Martino
KUZALIWA: Novemba 20, 1962 (Miaka 50), Rosario, Argentina
TIMU ya VIJANA: Newell's Old Boys
KLABU:
1980–1990 Newell's Old Boys Mechi 392 Magoli: 35
1991 Tenerife Mechi 15 Goli: 1
1991–1994 Newell's Old Boys Mechi: 81 Goli: 2
1994–1995 Lanús Mechi 30 Goli 3
1995 Newell's Old Boys Mechi 15
1996 Barcelona SC Mechi 5
ARGENTINA: Mechi 1
UMENEJA:
1998 Brown de Arrecifes
1999 Platense
2000 Instituto
2002–2003 Libertad
2003–2004 Cerro Porteño
2005 Colón
2005–2006 Libertad
2006–2011 Paraguay
2012–2013 Newell's Old Boys
2013- Barcelona FC
Gerardo Martino akiwa Fc Barcelona atakuwa
pamoja na Wasaidizi wake mwenyewe ambao ni Elvio Paolorrosso, Kocha wa
Viungo, na Msaidizi Jorge Pautasso.
Awali ilitegemewa Kiungo wa zamani wa
Barca, Luis Enrique, ndie atatwaa madaraka Nou Camp lakini tatizo kubwa
ni kuwa Enrique alijiunga na Klabu ya La Liga Celta Vigo Mwezi uliopita
tu na ukaja utata wa Mkataba.
Martino, au ‘Tata’ kama alivyo maarufu,
anakuwa Muargentina wa nne kuwa Kocha wa Barcelona wengine ni Helenio
Herrera, Roque Olsen na Cesar Luis Menotti na anatua Nuo Camp kuungana
na Supastaa wa Argentina Lionel Messi ambae amemsifia sana Kocha huyu.
Jumatano, Barcelona inacheza Mechi ya
Kirafiki na Mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich na itakuwa chini Jordi
Roura kwenye Mechi hiyo iatakayochezwa huko Allianz Arena, Munich.
Subscribe to:
Posts (Atom)