Nahodha wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya
miaka 20 (Ngorongoro Heroes), Aishi Manula amesema wamejipanga kwa ajili ya
kupata ushindi kwenye mechi dhidi ya Kenya itakayochezwa Jumapili (Aprili 6 mwaka
huu) katika mji wa Machakos.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo,
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yasoda akikabidhi
bendera hiyo, aliwataka wachezaji hao kujituma na kutanguliza uzalendo mbele
bila kusahau kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni ushirikiano.
Alisema Tanzania ina wachezaji wengi wenye vipaji,
hivyo waliopata fursa ya kuwemo Ngorongoro Heroes wakati huu wajue kuwa
wamepata bahati, na wanatakiwa kufahamu kuwa wao ni wawakilishi wa Tanzania, na
Watanzania wana kiu ya kusikia matokeo ya mechi hiyo.
Ngorongoro Heroes inayofundishwa na John Simkoko inaondoka kesho (Aprili
3 mwaka huu) saa 4.30 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways, na mara baada ya
kuwasili itakwenda moja kwa moja kwenye hoteli ya Garden iliyopo Machakos
ambayo ndiyo imepangiwa kufikia na Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF).
Wachezaji waliopo kwenye msafara huo unaoongozwa na
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF), Ayoub Nyenzi ni Abrahman Mohamed, Aishi
Manula, Ally Idd, Ally Mwale, Athanas Mdamu, Ayoub Semtawa, Bryson Raphael na
Edward Manyama.
Wengine ni Gadiel Michael, Hamad Juma, Hassan Mbande,
Ibrahim Ahmada, Idd Ally, Kelvin Friday, Michael Mpesa, Mohamed Ibrahim,
Mudhathir Yahya, Pato Ngonyani, Peter Manyika na Salum Mineli.
TIMU YA WATOTO WA MITAANI YACHACHAFYA BRAZIL
Timu ya
Watoto wa Mitaani ya Tanzania kutoka Kituo cha Mwanza inaendelea vizuri katika
mashindano ya Kombe la Dunia kwa Watoto wa Mitaani yanayoendelea Rio de Janeiro
nchini Brazil ambapo katika mchezo wake wa kwanza ilitoka sare ya mabao 2-2 na
Burundi.
Michuano
hiyo ya siku kumi inashirikisha timu kumi. Mbali ya Tanzania, nyingine ni
Argentina,
Burundi, India, Kenya, Liberia, Marekani, Mauritius, Misri na Pakistan. Kwa
wasichana ni Afrika Kusini, Brazil, El Salvador, Indonesia, Msumbiji,
Nicaragua, Philippines, Uingereza na Zimbabwe.