Wednesday, April 2, 2014

UCL:MAN UNITED YAOMYESHA UBABE DHIDI YA BAYERN MUNICH.

MABINGWA watetezi ligi ya Mabingwa Ulaya, Bayern Munich, jana Usiku wamefanikiwa kupambana na kupata Sare ya Bao 1-1 waliposhuka dimbani Uwanjani Old Trafford kupambana na Mabingwa wa England Man United katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Bayern kumaliza Mtu 10 baada ya Kiungo wao mahiri, Bastian Schweinsteiger, kutolewa kwa Kadi Nyekundu kufuatia Kadi za Njano mbili.
Bayern walimiliki sana Mpira katika Kipindi cha Kwanza lakini ni Man United ndio waliokosa nafasi ya wazi wakati Danny Welbeck alipobaki yeye na Kipa Neuer na kujaribu kufunga kiufundi lakini Kipa huyo wa Germany akaokoa Bao la wazi.
Mapema kwenye Dakika ya 3, Welbeck alifanikiwa kufunga Bao safi lakini Refa Carlos Velasco Carballo kutoka Spain alilikataa na kuwaacha Wachambuzi wengi kukuna vichwa vyao kwanini Bao hilo lilikataliwa.
Hadi Mapumziko Mechi hii ilikuwa 0-0.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 58, Man United walifunga Bao kwa Kichwa cha Nahodha wao Nemanja Vidic baada kuunganisha Kona ya Wayne Rooney.
Bayern walisawazisha katika Dakika ya 66 baada ya Krosi ya kumkuta Mario Mandzukic aliemsogezea Bastian Schweinsteiger na kufunga.
Katika Mechi ya Marudiano, mbali ya kumkosa Bastian Schweinsteiger pia itamkosa Javi Martinez baada Mchezaji huyo kuzoa Kadi ya Njano ambayo itamfanya akose Mechi ya Marudiano.
Timu hizi zitarudiana huko Allianz Arena Jijini Munich hapo Jumatano Aprili 9.
VIKOSI:
MANCHESTER UNITED: De Gea; Jones, Ferdinand, Vidic, Büttner; Valencia, Carrick, Fellaini, Giggs, Welbeck; Rooney
Akiba: Lindegaard, Hernandez, Nani, Young, Fletcher, Januzaj, Kagawa.
BAYERN MUNICH: Neuer; Rafinha, Boateng, Martinez, Alaba; Lahm; Robben, Kroos, Schweinsteiger, Ribéry; Muller
Akiba: Starke, Van Buyten, Mandzukic, Shaqiri, Pizarro, Gotze, Hojbjerg.
REFA: Carlos Velasco Carballo (Spain).
Robo Fainali
Mechi za Kwanza
Jumanne Aprili 1
Barcelona 1 Atletico Madrid 1
Manchester United 1 Bayern Munich 1
Katika mtanange mwingine usiku wa jana kwa mara ya 4 Msimu huu, Barcelona na Atletico Madrid zimetoka tena Sare ya bao 1-1 Uwanjani Nou Camp katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Licha ya Barca kutawala Kipindi cha Kwanza, hadi Mapumziko Bao zilikuwa 0-0 na kila Timu ilipata pigo baada kupata Majeruhi kwa Barca kulazimika kumtoa Pique na kumuingiza Bartra na Atletico kumtoa Diego Costa na Ribas Diego kuwa mbadala.
Kipindi cha Pili, Atletico walitangulia kuingia wavuni katika Dakika ya 57 kwa Bao la Ribas Diego na Neymar kusawazisha katika Dakika ya 71.
Timu hizi zitarudiana huko Estadio Vicente Calderon hapo Jumatano Aprili 9.
 VIKOSI:
BARCELONA: Pinto; Alves, Piqué, Mascherano, Alba; Busquets, Xavi; Cesc, Iniesta, Neymar; Messi
Akiba: Oier, Adriano, Song, Bartra, Sergi Roberto, Alexis, Pedro.
ATLÉTICO MADRID: Courtois; Juanfran, Godin Miranda, Filipe Luis; Tiago, Gabi; Arda Turan, Villa, Koke; Diego Costa
Akiba: Aranzubia, Alderweireld, Insua, Mario Suarez, Cristian Rodriguez, Sosa, Diego.
REFA: Felix Brych (Germany)
Jumatano Aprili 2
Real Madrid v Borussia Dortmund
Paris Saint-Germain v Chelsea
Marudiano
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Jumanne Aprili 8
Chelsea v Paris Saint-Germain
Borussia Dortmund v Real Madrid
Jumatano Aprili 9
-DROO YA NUSU FAINALI: 11 Aprili
-Mechi kuchezwa 22 & 23 Aprili na Marudiano 29 & 30 Aprili
-FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014.
WASHINDI [Miaka ya karibu]:
MSIMU MSHINDI NCHI MSHINDI WA PILI NCHI GOLI
2012-13 Bayern Munich Germany Borussia Dortmund Germany 2-1
2011-12 Chelsea England Bayern Munich Germany 1-1 (4–3)
2010-11 Barcelona Spain Manchester United England 3-1
2009-10 Internazionale Italy Bayern Munich Germany 2-0
2008-09 Barcelona Spain Manchester United England 2-0
2007-08 Man United England Chelsea England 1-1 (6–5)
UEFA CHAMPIONZ LIGI
WAFUNGAJI BORA 2013/14:
C. Ronaldo-Real Madrid Goli 13
Zlatan Ibrahimovic-PSG Goli 10 [Penati 1]
Messi-Barcelona Goli 8 [Penati 2]
Diego Costa-Atletico Madrid Goli 7
Sergio Agüero-Manchester City Goli 6 [Penati 2]