ROBO FAINALI
Marudiano
Jumatano Aprili 9
{Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili}
Bayern Munich 3 Manchester United 1 [4-2]
Atletico Madrid 1 Barcelona 0 [2-1]

Katika Mtange wa Kwanza huko Old Trafford Wiki iliyopita, Timu hizi zilitoka Sare ya Bao 1-1.
Kwenye Mechi hii, Man United
walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 57 la Patrice Evra lakini
Bayern walijibu haraka na kusawazisha Dakika 2 baadae kwa Bao la Mario
Mandzukic na kuongeza Bao mbili kupitia Thomas Muller, Dakika ya 68 na
Arjen Robben, Dakika ya 76.
Bayern sasa wanaungana kwenye Nusu Fainali ya UCL pamoja na Chelsea, Atletico Madrid na Real Madrid.
Droo ya kupanga Mechi za Nusu Fainali itafanyika Ijumaa Aprili 11.
VIKOSI:
BAYERN MUNICH: Neuer, Dante, Ribery, Mandzukic, Robben, Boateng, Gotze, Lahm, Muller, Alaba, Kroos.
Akiba: Raeder, Van Buyten, Rafinha, Pizarro, Weiser, Hojbjerg, Weihrauch.
MAN UNITED: De Gea; Jones, Smalling, Vidic, Evra; Fletcher, Carrick; Valencia, Rooney, Kagawa; Welbeck.
Akiba: Lindegaard, Büttner, Ferdinand, Giggs, Januzaj, Young, Hernandez.
REFA: Jonas Eriksson [Sweden]
Goli la Dakika ya 5 la Koke limewapa
ushindi Atletico Madrid wa Bao 1-0 dhidi ya Barcelona walipocheza
Uwanjani kwao Estadio Vicente Calderon katika Mechi ya Marudiano ya Robo
Fainali wa ligi ya mabingwa UCL,
katika mtanange wa awali timu hizi zilitoka Sare ya Bao 1-1 huko Nou Camp Wiki iliyopita.
Katika Mechi hiyo, Atletico walianza kwa
kishindo na mbali ya kufunga Bao hilo mapema pia walipiga Posti mara 3
ndani ya Dakika 20 za kwanza.
Hii ni mara ya kwanza kwa Atletico
kuingia Nusu Fainali ya Mashindano haya tangu Mwaka 1974 na ni mara ya
kwanza kwa Barca kushindwa kuingia Nusu Fainali tangu 2007.
Msimu huu, Timu hizi zimekutana mara 4 na kutoka Sare.
Atletico sasa wanaungana kwenye Nusu Fainali ya UCL pamoja na Chelsea, Bayern Munich na Real Madrid.
Droo ya kupanga Mechi za Nusu Fainali itafanyika Ijumaa Aprili 11.
VIKOSI:
VIKOSI:
Atletico Madrid: Courtois, Godin, Filipe Luis, Juanfran, Miranda, Tiago, Koke, Raul Garcia, Gabi, Adrian, Villa
Akiba: Aranzubia, Mario Suarez, Rodriguez, Alderweireld, Insua, Sosa, Diego.
Barcelona: Pinto, Mascherano, Bartra, Jordi Alba, Dani Alves, Fabregas, Xavi, Iniesta, Busquets, Messi, Neymar
Akiba: Oier, Montoya, Pedro, Alexis, Song, Adriano, Sergi Roberto.
REFA: Howard Webb [England]
UEFA CHAMPIONZ LIGI
ROBO FAINALI
Marudiano
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili]
Chelsea 2 Paris Saint-Germain 0 {3-3}, Chelsea wamesonga kwa Bao la Ugenini}
Borussia Dortmund 2 Real Madrid 0 {2-3}
DONDOO MUHIMU:
-DROO YA NUSU FAINALI: 11 Aprili
-Mechi kuchezwa 22 & 23 Aprili na Marudiano 29 & 30 Aprili
-FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014.
WASHINDI [Miaka ya karibu]:
MSIMU | MSHINDI | NCHI | MSHINDI WA PILI | NCHI | GOLI |
2012-13 | Bayern Munich | Germany | Borussia Dortmund | Germany | 2-1 |
2011-12 | Chelsea | England | Bayern Munich | Germany | 1-1 (4–3) |
2010-11 | Barcelona | Spain | Manchester United | England | 3-1 |
2009-10 | Internazionale | Italy | Bayern Munich | Germany | 2-0 |
2008-09 | Barcelona | Spain | Manchester United | England | 2-0 |
2007-08 | Man United | England | Chelsea | England | 1-1 (6–5) |