Monday, April 21, 2014

WANACHAMA WA CLUB YA COASTAL UNION WATOA NENO KUHUSU UONGOZI WAO.


Coastal union  ambayo imemaliza Ligi Kuu Bara ikishika nafasi ya tisa na alama 29 ambapo ilikuwa sio matarajio ya wanachama wa club hiyo nao wametoa neno.
Wanachama ambao wa club hiyo kutoka jiji la Tanga walitoa ujumbe kwa uongozi wao wakionyesha kupinga mambo kadhaa yanayoonekana kutokwenda sawa.
Lakini kilichoonyesha kweli mambo hayo hayako vizuri ni wachezaji kwenda kuwaunga mkono wanachama hao mara baada ya mechi hiyo kwisha.
Uongozi wa Coastal Union, umekuwa ukishutumiwa kukataa kutoa kadi mpya za wachama, huku Kassim El Siagi ambaye ni katibu mkuu akielezwa kuwa chanzo.
Siagi amekuwa akisisitiza kwamba lazima kabla ya kuwakubali wanachama wapya, basi wawahakiki kwanza kwa kuwajadili.
Lakini katiba ya Coastal Union haina kipengele hicho.

Saturday, April 19, 2014

ASHANT,JKT OLJORO, RHINO RANGERS MKONO WA KWAHERI ZASHUKA DARAJA



Ligi kuu Vodacom Tanzania bara leo imefikia tamati baada ya timu zote kusha dimbani katika viwanja saba hapa nchini ambapo Azam FC imekabidhiwa Kombe lao huko Azam Complex, Chamazi mara baada ya Mechi yao ya kukamilisha Ratiba ambayo waliifunga JKT Ruvu Bao 1-0.
Kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam, Watani wa Jadi, Yanga na Simba nao walikutana kwenye Dabi ya Kariakoo, isiyokuwa na maan
a yeyote mbali ya kukamilisha Ratiba, na kutoka Sare ya Bao 1-1.
Kwenye Mechi hiyo, iliyohudhuriwa na Watazamaji wachache tofauti na desturi, Simba walitangulia kufunga Bao katika Dakika ya 76 Mfungaji akiwa Haruna Chanongo na Yanga kusawazisha kwa Bao la Dakika ya 86 la Simon Msuva.
Mechi pekee iliyokuwa na umuhimu mkubwa ni ile iliyochezwa Uwanja wa Jamhri huko Morogoro kati ya Tanzania Prisons na Ashanti United na Prisons kuifunga Ashanti Bao 1-0 na wao kupona na kuishusha Daraja Ashanti ambao wa
naungana na JKT Oljoro na Rhino Rangers kuporomoka Daraja.
VPL, LIGI KUU VODACOM
Mechi za mwisho za Ligi
Ratiba/Matokeo:
Jumamosi Aprili 19
Rhino Rangers v Ruvu Shooting [Ali Hassan Mwinyi, Tabora]
Mbeya City 1 Mgambo JKT 0 [Sokoine, Mbeya]
Tanzania Prisons 1 Ashanti United 0 [Jamhuri, Morogoro]
JKT Ruvu 0 Azam FC [Azam 1 Complex, Chamazi]
JKT Oljoro 1 Mtibwa Sugar 1 [Sheikh Amri Abeid, Arusha]
Coastal Union 0 Kagera Sugar 1 [Mkwakwani, Tanga]
Yanga 1 Simba 1 [National Stadium, Dar es Salaam]
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Azam FC
26
18
8
0
51
15
36
62
2
Young Africans
26
16
8
2
61
19
42
56
3
Mbeya City
26
13
10
3
33
20
13
49
4
Simba SC
26
9
11
6
41
27
14
38
5
Kagera Sugar
26
9
11
6
23
20
3
38
6
Ruvu Shooting
25
9
8
8
26
32
-6
35
7
Mtibwa Sugar
26
7
10
9
30
31
-1
31
8
JKT Ruvu
26
10
1
15
23
40
-17
31
9
Coastal Union
26
6
11
9
17
20
-3
29
10
Mgambo JKT
26
6
8
12
18
35
-17
26
11
Tanzania Prisons
26
6
10
10
26
33
-7
28
12
Ashanti United
26
6
7
13
20
39
-19
25
13
JKT Oljoro
26
3
10
13
19
37
-18
19
14
Rhino Rangers
25
3
7
15
18
37
-19
16