Monday, May 12, 2014

STARS, ZIMBABWE KUUMANA DAR JUMAPILI

Mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika 2015 nchini Morocco kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe (Mighty Warriors) itafanyika Jumapili (Mei 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
UWANJA_WA_TAIFA_DAR
Awali mechi hiyo tulipanga ichezwe Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kwa nia ya kuhakikisha mikoa yote ya Tanzania inapata fursa ya kuwa mwenyeji wa mechi za kimataifa.
Ili Uwanja wa Sokoine uweze kuchezwa mechi za kimataifa za mashindano, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) lilituma Mkaguzi (inspector) wake kwenye uwanja huo Jumamosi (Mei 10 mwaka huu) ambapo imeamua kuwa marekebisho yanayofanyika hayatamalizika katika muda stahili, hivyo mchezo huo kutochezwa Sokoine.
Tunatoa mwito kwa wamiliki wote wa viwanja kuwasiliana na TFF ili Idara ya Ufundi iwaelekeze maboresho ya kufanya ili viwanja vingi iwezekanavyo viweze kukidhi viwango vinavyotakiwa na CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Taifa Stars ambayo ilikuwa kambini mkoani Mbeya itarejea Dar es Salaam keshokutwa (Mei 14 mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo.
BONIFACE WAMBURA 
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (T

Sunday, May 11, 2014

NIGERIA YAITANDIKA 2-0 NGORONGORO HEROES TAIFA

Timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20,Ngorongoro Heroes jioni hii imeambulia kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Nigeria uwanja wa taifa jijini dare s salaam katika Mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wa 20 ambapo kwa matokeo hayo yamempa kazi ngumu kocha mkuu John Simkoko kusonga mbele.
Ngorongora walipata nafasi kadhaa za kufunga kipindi cha kwanza, lakini bado ugonjwa wa kutotumia nafasi muhimu unazidi kuitafuna timu hii

Mshambuliaji Saady Kipanga alishindwa kuonesha makeke yake baada ya kupoteza nafasi kadhaa za kufunga.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika milango ya timu zote ilikuwa migumu, huku kipa namba moja wa Heroes, Aishi Manula akiumia.
Kipindi cha pili, Manula alishindwa kurejea uwanjani na kumpisha kipa namba mbili, Peter Manyika.
Katika Kipindi hicho cha pili Ngorongoro waliingia kizembe na kujikuta wakifungwa mabao mawili na kumaliza mechi kwa kipigo cha nyumbani cha mabao mawili kwa sifuri.

RAMBIRAMBI MSIBA WA BALOZI WA MALAWI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha Balozi wa Malawi nchini, Flossie Gomile-Chidyaonga kilichotokea juzi (Mei 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

RUVU SHOOTING YAMNASA MCHEZAJI TOKA KAGERA SUGAR.

Club ya Ruvu Shooting ya mkoani  pwani imefanikiwa kumnsa mchezaji mahiri wa timu ya Kagera sugar nafasi ya midfild kwa kipindi cha misimu miwili iliyopita, Zuberi Kasim Dabi ambapo amesaini dili la  mkataba wa miaka miwili kuichezea timu  hiyo ya Pwani.
Dabi amesaini mkataba huo Ijumaa hii, Mei 9, 2014 katika ofisi za Ruvu shooting zilizoko Mlandizi, Pwani mbele ya uongozi wa timu hiyo ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Kanali Charles Mbuge.
Dabi kabla ya kujiunga na Kagera sugar amewahi pia kuzichezea timu za Villa Squad ya Dar es salaam, Polisi Morogoro ambayo musimu huu imefanikiwa kupanda daraja, kucheza ligi kuu.
Ruvu shooting ipo katika mchakato mkali na mkubwa kukisuka kikosi chake kwa kusajili wachezaji wenye uwezo kama kocha wake mkuu Tom Olaba alivyoshauri.
Wakati Ruvu shooting wakisajili wachezaji wa timu kubwa, tayari kikosi hicho kimeivunja timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 na kutangaza kukiunda upya kwa kuwafanyia majaribio wachezaji vijana kati ya Mei 15-28, majaribio ambayo yatafanyika katika uwanja wa Mabatini, Mlandizi

M/KITI WA YANGA YUSUPH MANJI AUNGURUMA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI.


Mwenyekiti wa Young Africans Bw Yusuf Manji akiongea na wanachama, wazee na waandishi wa habari leo makuu ya klabu ya Yanga
Mwenyekiti wa Young Africans Bw Yusuf Manji amesema kuondoka kwa wachezaji wao wawili Didier Kavumbagu na Frank Domayo sio mwisho wa timu ya Yanga, kwani uongozi wake unaendelea na mipango ya kuhakikisha inasajli wachezaji wengine wazuri ambao wataisadia timu kwenye msimu ujao kwa kufuata maelekezo ya Benchi la Ufundi.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu leo, Manji amesema yameongelewa mengi sana kwa kipindi cha mwezi mmoja ambao hakuwepo nchini kwa ajili ya kazi zake binafsi lakini sasa amerejea na maandalizi ya msimu ujao yameshaanza.
Kuondoka kwa Kavumbagu ni kutokana na kuchelewa kwa majibu ya TFF juu ya idadi ya wachezaji wageni kwa msimu mpya, huku Domayo ambae tangu mwaka jana aliombwa kuongeza mkataba alikua akisema anamsubiria mjomba wake ndipo aweze kufanya hivyo.
Pamoja na kuondoka kwa wachezaji hao bado kwa kushirikiana na kocha Hans watahakikisha Yanga inaendelea kutisha msimu ujao na kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa, Hans aliahidi kuleta wachezaji wazuri watakaoisaidia Yanga siku alipokua akiiongea na waandishi wa habari kuwaaga.
Aidha Manji amelifuta rasmi tawi la Tandale kutokana na kuwa na chanzo cha vurugu na migogoro ndani ya klabu, pia amewafuta uanachama wanachama sita ambao walikiuka katiba ya Yanga kwa kwenda kuongea na waandishi na HABARI bila ya Idhini ya uongozi huku pia wakishindwa kulipia ada zao za uanachama kwa zaidi ya miezi sita, waliofutwa uanachama ni:
1. Ally Kamtande, 2. Isiaka Dude, 3. Hamisi Matandula, 4.Waziri Jitu Ramadhani, 5.Mohamed Kigali Ndimba , 6. Selaman Hassan Migali 
Mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba utafanyika terehe mosi Juni, 2014 katika Ukumbi wa Oysterbay Police Mess na wanachama wote wanaombwa kulipia ada zao ili waweze kuhuhudhira mkutano huo wakiwa hai. 
Suala la ujenzi wa Uwanja wa Kisasa eneo la Jangwani bado lipo pale pale, kikubwa kinachosubirwa ni majibu ya serikali juu ya maombi ya eneo la ziada, kwani Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alisema suala hilo lipo ukingoni na mda si mrefu.

Friday, May 9, 2014

MAKOCHA NGORONGORO HEROES, EAGLES KUTETA

Makocha wa timu za Tanzania (Ngorongoro Heroes), John Simkoko na Nigeria (Flying Eagles), Manu Garba wanakutana na waandishi wa habari kuzungumzia mikakati yao kwa ajili ya mechi ya Jumapili.

IMG_8599Mkutano huo utafanyika kesho (Mei 10 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuanzia saa 5 kamili asubuhi.
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 itafanyika Jumapili (Mei 11 mwaka huu) saa 10 kamili jioni katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

RCL YAANZA KUTIMUA VUMBI KATIKA VITUO VITATU

Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayoshirikisha timu 27 inaanza kutimua vumbi kesho (Mei 10 mwaka huu) katika vituo vitatu vya Morogoro, Mbeya na Shinyanga kwa mechi mbili kila siku.
Kundi A ambalo mechi zake zinachezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, African Sports ya Tanga itacheza na Kiluvya United FC ya Pwani saa 8 mchana wakati saa 10 jioni ni Mji Mkuu FC (CDA) ya Dodoma dhidi ya Pachoto Shooting Stars ya Mtwara.
Ligi-ya-MkoaJumapili (Mei 11 mwaka huu) katika kundi hilo kutakuwa na mechi kati ya Bulyanhulu FC (Shinyanga) na Kariakoo SC (Lindi) itakayoanza saa 8 mchana wakati saa 10 jioni ni Navy FC (Dar es Salaam) na Abajalo FC pia ya Dar es Salaam.
Kundi B katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya litaanza ligi kwa mechi kati ya Ujenzi (Rukwa) na Volcano FC (Morogoro) saa 8 mchana wakati saa 10 jioni ni AFC ya Arusha na Panone FC ya Kilimanjaro.
Mei 11 mwaka huu saa 8 mchana ni Mpanda United ya Katavi na Magereza ya Iringa wakati Tanzanite (Manyara) na Njombe Mji (Njombe) zenyewe zitaumana kuanzia saa 10 jioni.
Simiyu United ya Simiyu na Mvuvumwa FC (Kigoma) ndizo zitakazoanza kucheza saa 8 mchana katika kundi C linalotumia Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Saa 10 jioni ni mechi kati ya Wenda FC ya Mbeya na mabingwa wa Mkoa wa Kagera, Eleven Stars FC.
Jumapili (Mei 11 mwaka huu), mechi za kundi hilo zitakuwa Singida United (Singida) na Mbao FC ya Mwanza kuanzia saa 8 mchana wakati jioni ni pambano kati ya mabingwa wa Mkoa wa Mara, JKT Rwamkoma FC na Geita Veterans FC ya Geita.
Ligi hiyo itamalizika Juni 2 mwaka huu ambapo timu itakayoongoza kila kundi itapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015.