Gareth Bale
|
|||
Kuhusu yeye binafsi
|
|||
Full name
|
Gareth Frank Bale
|
||
Date of birth
|
|||
Place of birth
|
Cardiff, Wales
|
||
Height
|
|||
Playing position
|
|||
Timu ya sasa
|
|||
Current team
|
|||
Number
|
11
|
||
Timu za Vijana
|
|||
–
|
|||
2005–2006
|
|||
Timu za ukubwa
|
|||
Years
|
Team
|
Mechi
|
(Goli)
|
2006–2007
|
40
|
(5)
|
|
2007–2013
|
146
|
(42)
|
|
2013–
|
27
|
(15)
|
|
Timu ya Taifa
|
|||
2005–2006
|
7
|
(1)
|
|
2006
|
1
|
(1)
|
|
2006–2008
|
4
|
(2)
|
|
2006–
|
44
|
(12)
|
Wednesday, July 16, 2014
GARETH BALE LEO ATIMIZA MIAKA 25 AKIWA NDANI YA REAL MADRID
AFRIKA KUSINI YAWASILI KUIVAA SERENGETI BOYS

Timu hiyo yenye msafara wa watu 37
ilitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku
(Julai 15 mwaka huu) na imefikia hoteli ya Sapphire. Amajimbos itafanya
mazoezi leo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Waamuzi watakaochezesha mechi hiyo
kutoka Shelisheli wakiongozwa na Allister Barra tayari wamewasili
nchini. Kamishna wa mechi hiyo ni Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy
kutoka Madagascar.
Makocha wa timu za Seregenti Boys
na Amajimbos pamoja na manahodha wao watakuwa na mkutano na waandishi wa
habari kesho (Julai 17 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kiingilio katika mechi hiyo ni sh. 2,000. Tiketi zitauzwa uwanjani katika magari maalumu siku ya mechi.
SAMATA, ULIMWENGU WATUA, MWINYI KAZIMOTO KESHO
Washambuliaji Mbwana Samata na
Thomas Ulimwengu wamewasili nchini leo asubuhi (Julai 16 mwaka huu)
kutoka Tunisia kujiunga na Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya
Msumbiji itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji hao wamefikia hoteli ya
Courtyard, Seaview Upanga na leo (Julai 16 mwaka huu) watafanya mazoezi
kwa programu maalumu waliyopewa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij
wakati wakiwasubiri wenzao.

Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager itawasili Dar es Salaam kesho (Julai 17 mwaka
huu) saa 3.20 asubuhi kwa ndege ya Fastjet kutoka Mbeya tayari kwa
maandalizi ya mwisho kabla ya kuivaa Msumbiji.
RAIS MALINZI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa
habari Ijumaa (Julai 18 mwaka huu).
Thursday, July 10, 2014
SIMBA YAMNASA HUSSEIN SHARRIF KUTOKA MTIBWA
Simba Wekundu wa Msimbazi, Simba wamekamilisha usajili wa kipa
namba moja wa Mtibwa Sugar, Hussein Sharrif
`Iker Casillas` na kumsainisha mkataba wa miaka miwili.
Casillas aliyekuwa tegemeo
katika klabu ya Mtibwa Sugar ameungana na makipa Ivo Mapunda na Abuu
Hashim katika kikosi cha Simba.
SERENGETI BOYZ VS AFRICA KUSINI AZAM COMPLEX
Timu ya Taifa ya vijana
wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boyz) inacheza mechi ya kujipima
nguvu kesho (Julai 11 mwaka huu) dhidi ya Azam U-20 kwenyeUwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mechi hiyo ambayo ni maalumu kwa
benchi la ufundi la Serengeti Boyz likiongozwa na kocha Hababuu Ali
Omari kuangalia kikosi chao itaanza saa 2 kamili asubuhi.
Serengeti Boyz itacheza mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika
dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos) siku ya Ijumaa, Julai 18 mwaka huu
kwenye uwanja huo huo wa Azam Complex kuanzia saa 10 kamili jioni.
Wachezaji wanaounda kikosi cha
Serengeti Boyz ni Abdallah Shimba, Abdulrasul Bitebo, Abutwalibu Mshery,
Adolf Bitegeko, Ally Mabuyu, Ally Mnasi, Amin Noren, Athanas Mdamu,
Badru Othman, Baraka Baraka, Hatibu Munishi na Issa Athuman.
Wengine ni Juma Yusuf, Kelvin Faru, Kelvin Kamalamo, Martin
Luseke, Mashaka Ngajilo, Mechata Mnata, Mohamed Abdallah, Mussa Vicent,
Nazir Barugire, Omary Omary, Omary Wayne, Prosper Mushi, Seif Seif na
Yahya Hafidh.
Subscribe to:
Posts (Atom)