Tuesday, November 4, 2014

LIGI KUU VODACOM:WIKIENDI YA JUMAMOSI MOTO KUWAKA TENA KATIKA ROUNDI YA 7

     
Ligi kuu vodacom ta tanzania bara  itaingia katika Raundi ya 7 Wikiendi hii katika viwanja tofautitofauti nchini ambapo mechi za wiki hii:

 RATIBA VPL:
Jumamosi Novemba 8
Stand United v Mbeya City
Yanga v Mgambo JKT                
Stand United v Mbeya City  
Mtibwa Sugar v Kagera Sugar               
Azam FC v Coastal Union           
Polisi Moro v Prisons
Jumamosi Novemba 8
Simba v Ruvu Shootings             
JKT Ruvu v Ndanda FC
Ijumaa Desemba 26
Simba v Kagera Sugar

Jumamosi Desemba 27
Mtibwa Sugar v Stand United               
Prisons v Coastal Union             
JKT Ruvu v Ruvu Shootings
Jumapili Desemba 28
Mbeya City v Ndanda FC            
Polisi Moro v Mgambo JKT          
Yanga v Azam FC             
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Mtibwa Sugar
6
4
2
0
9
2
7
14
2
Coastal Union
6
3
2
1
7
4
3
11
3
Azam FC
6
3
1
2
6
3
3
10
4
Yanga
6
3
1
2
7
5
2
10
5
Kagera Sugar
6
2
3
1
4
2
1
9
6
Mgambo JKT
5
3
0
3
4
5
-1
9
7
JKT Ruvu
6
2
1
3
5
7
-2
7
8
Ruvu Shooting
6
2
1
3
4
6
-2
7
9
Simba
6
0
6
0
6
6
0
6
10
Tanzania Prisons
6
1
3
2
5
5
0
6
11
Ndanda FC
6
2
0
4
8
10
-2
6
12
Polisi Moro
6
2
2
2
5
7
-2
6
13
Stand United
6
1
3
2
4
9
-8
6
14
Mbeya City
6
1
2
3
3
4
-1
5

RAIS WA BARCA BARTOMEU AKANUSHA BARCELONA KUWA NA MGOGORO.

RAIS wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu amesisitiza kuwa hakuna mgogoro wowote Camp Nou na kudai kocha Luis Enrique bado anaungwa mkono na klabu hiyo.
Baada ya kuanza vyema msimu wa La Liga, Barcelona walijikuta wakiteleza kutoka nafasi ya kwanza mpaka ya nne katika msimamo wa ligi kufuatia vipigo viwili mfululizo dhidi ya Real Madrid na Celta Vigo.

Kumekuwa na taarifa kutoka vyombo vya habari vya Hispania kuwa wachezaji nyota wa timu hiyo hawakufurahishwa na kikosi kilichoanza na mbinu walizoelekezwa wakati walipofungwa na mabao 3-1 na Madrid. 
Hata hivyo, Bartomeu amesema haamini kama kufungwa mechi mbili kutaleta tatizo lolote kwani bado wana imani kuwa Enrique ndiye mtu sahihi kwa kazi hiyo.

JE WAJUA KUFANYA KAZI USIKU KUNA MADHARA MAKUBWA

Wanasayansi wanasema kuwa kufanya kazi katika muda usio wa kawaida kikazi au katika mazingira yaliyo ya upweke kunaweza kuzeesha ubongo na kufanya uwezo wa utendaji kuwa duni.
Utafiti huo umeeleza katika jarida la Occupational and Environmental Medicine kuwa iwapo kazi za kupokezana, mfano nyakati za usiku zitafanywa kwa takriban miaka kumi mfululizo zitazeesha ubongo kabla ya wakati wake.
Wanasayansi wanasema ahueni imeonekana kwa watu baada ya kuacha kufanya kazi hizo lakini ilichukua miaka mitano kurejea kwenye hali ya kawaida.
Utafiti huu unaelezwa kuwa muhimu, kwa kuwa waathiriwa wengi kutokana na tatizo hilo wamekuwa wakilala usingizi wa mang'amung'amu
Moja ya madhara yatokanayo na kufanya kazi usiku ni kuongezeka uzito kupita kiasi                    
Wataalam hawa wameiambia BBC kuwa miili na akili zimejengwa kwa kufanya kazi mchana na kulala nyakati za usiku.
Athari mbaya ambazo zinaelezwa kutokana na mtindo huo wa ufanyaji kazi ni madhara ya Saratani na uzito mkubwa.
Timu ya wanasayansi kutoka chuo cha Swansea na Toulouse wameonesha kuwa kuna madhara ya kiakili pia.

RASMI:KALI ONGALA WA AZAM FC ACHIA NGAZI KUIFUNDISHA TIMU HIYO

Kocha msaidizi wa azam Fc kali Ongala ameachia ngazi kuifundisha klabu hiyo kwa sababu ya kwenda nchini England kuendelea na masomo.
Jafari iddy Maganga Ofisa Habari wa klabu hiyo amesema kocha huyo amekuwa akishiriki kozi fupi fupi za ukocha kwa muda mrefu nchini humo,lakini sasa ameamua kuomba uongozi wa klabu hiyo muda mrefu wa kwenda kasoma masomo hayo yatakayochukuwa muda mrefu.
Jaffari iddy amekanusha taarifa za kocha huyo kuachia ngazi kwa sababu ya kutoelewana na klabu hiyo baada ya matokeo yasiyolizisha.
Kali alisajiliwa mwaka 2009 kama mchezaji wa ndani akitokea nchini Sweden na baadaye aliondoka nchini Uingereza kwa ajili ya kusomea ukocha na kurejea akiwa kocha msaidizi wa timu hiyo.