Thursday, June 20, 2013

BRAZIL YAFANYA KWELI KOMBE LA MABARA-

TIMU ya taifa ya Brazil imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi yake ya pili ya Kombe la Mabara ambapo mshambuliaji mpya wa FC Barcelona Neymar akiifungia  timu yake bao  safi kunako dakika ya 10 ya kipindi cha kwanza kabla ya kumtengenezea nafasi ya kufunga bao la pili Jo.
Brazil imeichalaza Mexico mabao 2-0 ambapo sasa imefanikiwa kufikisha ponti sita na kuzidi kuziweka katika nafasi nzuri na kuongoza Kundi A.
katika goli hili hilo Daniel Alves alipiga krosi  safi kutoka kulia ambapo ilimfikia Neymar akaitokea kwa mbele ya beki wa Mexico, kabla ya kuhadaa na kumtungua kipa Jose Corona dakika ya tisa na dakika ya 90 akampa pande Jo kufunga la pili.
Katika mchezo huo uliokuwa chini refa Howard Webb wa Uingereza, kikosi cha Brazil kilikuwa: Cesar, Alves, Silva, Luiz, Marcelo, Luiz Gustavo, Paulinho, Oscar/Hernanes dk62, Hulk/Lucas Moura dk78, Neymar na Fred. 
Mexico: Corona, Rodriguez, Salcido,  Torrado, Dos Santos, Henandez, Moreno,  Guardado, Torres/Barrera dk70, Mier na Flores/Herrera dk68.
MSIMAMO KUNDI A
NA
TIMU
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Brazil
2
 2
0
0
  5
 0
  5
 6
2
Italy
2
 2
0
0
  6
 4
  2
 6
3
Mexico
2
 0
0
2
 1
 4
 -3
 0
4
Japan
2
 0
0
2
 3
  7
 -4
 0
MSIMAMO KUNDI B
NA
TIMU
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Nigeria
1
 1
0
0
 6
 1
 5
 3
2
Hispain
1
 1
0
0
 2
 1
 1
 3
3
Uruguay
1
 0
0
1
 1
 2
-1
 0
4
Tahiti
1
 0
0
1
 1
 6
 -5
 0
RATIBA LEO 
Alhamis Juni 20
Saa 4 usiku
Spain vs Tahiti
 Saa 7 usiku
Nigeria vs Uruguay 

TAFAKARI YA LEO NA EDEN HAZARD KATIKA HARAKATI ZA ULIMWENGU WA SOKA.

TAARIFA KUHUSU YEYE
Full nameEden Hazard
Date of birth7 January 1991 (age 22)
Place of birthLa Louvière, Belgium
Height1.70 m (5 ft 7 in)
Playing positionWinger
TAARIFA KUHUSU CLUB
Timu ya sasaChelsea
Number17
TIMU ZA UJANA
1995–2003Royal Stade Brainois
2003–2005Tubize
2005–2007Lille
TIMU ZA UJANA
MwakaTimuMechiGoli
2007–2012Lille147(36)
2012–Chelsea34(9)
TIMU YA TAIFA
2006Belgium U155(1)
2006Belgium U164(2)
2006–2008Belgium U1717(2)
2007–2009Belgium U1911(6)
2008–Belgium37(5)

TUZO NA VILABU
Lille fc
Ligue 1 (1): 2010-11
Coupe de France (1): 2010-11
Chelsea 
UEFA Europa Ligi (1): 2012-13
TUZO BINAFSI
UNFP Ligue 1 Mchezaji wa Mwaka (2): 2010-11, 2011-12
UNFP Ligue 1 Mchezaji  kijana wa Mwaka (2): 2008-09, 2009-10
UNFP Ligue 1 Timu ya Mwaka (3): 2009-10, 2010-11, 2011-12
UNFP Mchezaji wa Mwezi (3): Machi 2010, Machi 2011, [221] Machi 2012
Ligi Kuu ya PFA Timu ya Mwaka (1): 2012-13
Bravo tuzo (1): 2011 

SERENA WILLIAMS AOMBA RADHI KATIKA GAZETI"

Mwanariadha nyota wa kike mahiri katika mchezo wa tenisi anayeshika namba moja katika orodha za ubora duniani kwa upande wanawake, Serena Williams ameomba radhi kwa kauli aliyoitoa katika gazeti la Rolling Stone kuhusiana na kesi ya ubakaji. Nyota huyo ambaye anatarajiwa kutetea ubingwa wake wa michuano ya Wimbledon alikaririwa na gezeti kuhusiana na kesi hiyo inayoendelea katika mji wa Steubenville, Ohio, Marekani. Katika kesi hiyo wachezaji wawili wa mpira wa miguu wa kimarekani wanatuhumiwa kumbaka msichana aliyelewa mwenye umri wa miaka 16 tukio ambalo walilifanya Machi mwaka huu. Gazeti hilo la Rolling Stone lilimkariri Williams akidai kuwa hamlaumu msichana huyo lakini kama una umri wa miaka 16 na unakunywa kiasi hicho wazazi wako wanatakiwa kukufundisha kwamba usipokee kinywaji kutoka kwa mtu usiyemfahamu.Kauli yake hilo ilishambuliwa na watu mbalimbali nchini humo mpaka kupelekea nyota kuomba radhi akidai kuwa hakumaanisha kama watu wanavyofikiri.

ANZHI MAKHACHKALA KUFUNGIWA NA UEFA.

Timu ya soka ya Anzhi Makhachkala ya Urusi kwa mara nyingine haitacheza mechi zake za Europa League msimu ujao mbali na uwanja wao wa nyumbani baada ya kufungiwa na Shirikisho la Soka barani-UEFA humo kwasababu za kiusalama. Katika taarifa ya UEFA iliyotumwa katika mtandao wake imedai kuwa baada ya kufanya utafiti wa usalama katika mji wa Kaskazini wa Caucasus ambao klabu hiyo inatoka wamegundua kuwepo usalama mdogo hivyo hawatoruhusu timu hiyo kucheza mechi zake nyumbani. UEFA imeitaka klabu hiyo kutafuta uwanja mbadala kwa ajili ya mechi zake za nyumbani za Europa League msimu wa 2013-2014. Anzhi walimaliza katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Urusi msimu uliopita na kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. 

Wednesday, June 19, 2013

BPL HADHARANI MAN U KUUMANA NA SWANSEA CITY

HATIMAYE RATIBA ya Ligi Kuu nchini Uingereza BPL kwa ajili ya msimu wa 2013-2014 imetoka huku mabingwa wa ligi hiyo Manchester United wakipangwa kufungua msimu na timu ya Swansea City. Ratiba hiyo itamshuhudia David Moyes akianza kibarua chake katika mechi ya kwanza kama bosi wa United dhidi ya timu hiyohiyo ambayo Sir Alex Ferguson alikutana nayo katika mchezo wake wa mwisho kabla ya kustaafu. Washindi wa pili wa ligi hiyo Manchester City watawakaribisha Newcastle United wakati Hull City ambayo imepanda daraja msimu huu itakuwa na safari ngumu pale watakapoifuata Chelsea, Stamford Bridge. Mechi nyingine Crystal Palace ambao nao wamepanda daraja msimu huu watawakaribisha Tottenham Hotspurs katika mchezo wa mahasimu wa jijini la London huku Arsenal wakiwakaribisha Aston Villa wakati Stoke City watakuwa wenyeji wa Liverpool. Nyingine ni Norwich watakuwa wenyeji wa Everton, Sunderland watakwaana na Fulham, West Bromwich na Southampton huku West Ham United wakichuana na Cardiff City.

PUYOL MBIONI KUFANYI UPOASUAJI WA GOTI LAKE"

Beki mahiri na mwenye nguvu za kukaba wa klabu ya Barcelona, Carles Puyol anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa goti lake la kulia ambao utamuweka nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu mpaka nne. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa katika mtandao wa klabu hiyo mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania anatarajiwa kufanyiwa upasuaji huo leo. Puyol mwenye umri wa miaka 35 amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara katika miaka ya karibuni ukiwemo upasuaji wa mguu huohuo mara mbili, kuvunjika mfupa wa taya na pia kuteuka kiwiko cha mkono wake. Majeraha hayo yalimlazimu nyota huyo kukosa michuano ya Euro 2012 ambapo Hispania walitawadhwa mabingwa kwa mara ya pili mfululizo na pia kuenguliwa katika kikosi cha nchi hiyo kilichopo nchini Brazil kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho.

FABRIGAS AFUNGUKA KUHUSU REAL MADRID-USAJILI BALE

Kiungo nyota wa klabu ya Barcelona  na timu ya Tifa ya hispain Cesc Fabregas ametanabisha kuwa klabu ya Real Madrid ya Hispania watakuwa wametwanga maji kwenye kinu mtungi endapo kama wakivunja rekodi ya usajili kwa kulipa euro milioni kwa kumsajili mshambuliaji nyota wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Gareth Bale. ambaye ni Mshambuliaji  nyota wa kimataifa wa Wales amekuwa akihusishwa kwenda Santiago Bernabeu huku kukiwa na tetesi kuwa ada ya uhamisho wake inafikia paundi milioni 85 ambayo itavunja rekodi ya sasa ya euro milioni 94 ambazo Madrid aliipa Manchester United kwa ajili ya Cristiano Ronaldo. Hatahivyo, Fabregas haelewi kwanini klabu hiyo inajiandaa kulipa kiasi hicho kikubwa cha pesa huku wakijua kuwa kuna tatizo kubwa la mdodoro wa kiuchumi unaizikumba baadhi ya nchi wakiwemo wao. Fabregas pia alirejea kauli yake kwamba angependa kuendelea kubakia Barcelona na kushangaa baadhi ya watu wakizungumza kwamba anataka kurejea katika Ligi Kuu nchini Uingereza.