Kiungo nyota wa klabu ya Barcelona na timu ya Tifa ya hispain Cesc Fabregas ametanabisha kuwa klabu ya Real Madrid ya Hispania watakuwa wametwanga maji kwenye kinu mtungi endapo kama wakivunja rekodi ya usajili kwa kulipa euro milioni kwa kumsajili mshambuliaji nyota wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Gareth Bale. ambaye ni Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Wales amekuwa akihusishwa kwenda Santiago Bernabeu huku kukiwa na tetesi kuwa ada ya uhamisho wake inafikia paundi milioni 85 ambayo itavunja rekodi ya sasa ya euro milioni 94 ambazo Madrid aliipa Manchester United kwa ajili ya Cristiano Ronaldo. Hatahivyo, Fabregas haelewi kwanini klabu hiyo inajiandaa kulipa kiasi hicho kikubwa cha pesa huku wakijua kuwa kuna tatizo kubwa la mdodoro wa kiuchumi unaizikumba baadhi ya nchi wakiwemo wao. Fabregas pia alirejea kauli yake kwamba angependa kuendelea kubakia Barcelona na kushangaa baadhi ya watu wakizungumza kwamba anataka kurejea katika Ligi Kuu nchini Uingereza.