Andre Villas-Boas kocha wa Tottenham ameripotiwa kuitupilia mbali ofa ya kuifundisha club Paris Saint-Germain lengo kuu likiwa ni kubaki ndani ya White Hart Lane {Tottenham}.
Mabingwa hao wa Ufaransa walimhitaji AVB Mreno huyo kurithi mikoba ya Carlo Ancelotti ambaye anatarajiwa kuelekea nndani ya Bernebeu Real Madrid lakini sasa mawzo yote yamehamia kwa Fabio Capello.
Inafahamika Villas-Boas alipewa ofa ya Mkataba wa miaka mitatu na mabilionea wa Qatari wanaoimiliki PSG baada ya majadiliano na wakala wake, Carlos Goncalves, lakini mwalimu huyo kijana wa miaka 35 anataka kufanya mambo makubwa katika club ya Spurs ambapo walimchukuwa msimu uliopita akitokea katika club ya chelsea baada ya kutupiwa virago Chelsea.
Katika Taarifa za jana usiku nchini Ufaransa zimesema kuwa kocha wa zamani wa England, Capello atakuwa mwalimu mpya wa PSG kwa Mkataba wa mwaka mmoja.
Kocha wa zamani wa England, Capello anatazamiwa kuwa mpango B wa PSG, licha ya kwamba bado ana Mkataba wa mwaka mmoja Urusi.
Urusi ipo kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil,na kuna uwezekano Capello akarejea katika timu hiyo ya taifa baada ya msimu mmoja na PSG kukamilisha majukumu yake katika Kombe la Dunia.