Stoke City wamemsaini Beki wa Kimataifa wa Timu ya Spain U-21 Marc Muniesa anaecheza Barcelona kwa Uhamisho wa bure.
Muniesa, Miaka 21, ni mmoja wa Wachezaji
wa Spain ambayo ilitwaa Ubingwa wa EURO 2013 kwa U-21 hivi karibuni na
anajiunga na Stoke kwa Mkataba wa Miaka minne.
Huyu ni Mchezaji wa pili kuchukuliwa na
Meneja mpya wa Stoke, Mark Hughes, baada ya Wiki iliyopita kumsaini Erik
Pieters kutoka PSV Eindhoven.
SWANSEA YAKUBALIANA NA LIVERPOOL KUHUSU JONJO
Swansea City imeafikiana na Liverpool
Ada ya Pauni Milioni 6 ya kumhamisha Kiungo Jonjo Shelvey na Mchezaji
huyo sasa atakutana na Swansea ili kukamilisha makubaliano ya Maslahi
yake binafsi.
Jonjo Shelvey, Miaka 21, alisainiwa na
Liverpool kutoka Charlton Athletics kwa Dau la Pauni 1.7 Miaka mitatu
iliyopita lakini akiwa Anfield kupata namba kwake kumekuwa nadra na
Meneja Brendan Rodgers amemruhusu kutafuta Klabu nyingine.
Shelvey aliichezea England kwa mara ya
kwanza Novemba Mwaka jana ilipofungwa na Sweden na pia amecheza Mechi 17
za Ligi huko Anfield Msimu uliopita.
Jana Swansea ilitangaza kuwasaini
Wachezaji watatu wengine ambao ni Alejandro Pozuelo, Miaka 21, kutoka
Real Betis ya Spain, Kipa wa Miaka 17, Gregor Zabret kutoka Klabu ya
Slovenia NK Domzale na Alex Gogic, Kiungo wa Miaka 19 kutoka Klabu ya
Greece, Olympiakos.

Katika azma yao ya kukiimarisha Kikosi
chao kuwa na nguvu na Misuli inayostahili kwa ajili ya Msimu mpya, Klabu
ya Arsenal imemuajiri Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Ireland wa
Mchezo wa Raga, Jerry Flannery, kuwa Kocha wao mpya wa kujenga nguvu,
musili na stamina kwa Wachezaji wao.
Flannery, Miaka 34, alistaafu mapema kucheza Raga baada ya kuumia Misuli za Mguu.
MOURINHO AZUNGUMZA NA MARCO VAN GINKEL
Chelsea imefanya mazungumzo na Kiungo wa Vitesse Arnhem, Marco van Ginkel, ili ahamie Stamford Bridge.
Van Ginkel, Miaka 20, ameshakutana na Jose Mourinho na Alhamisi ataongea na Klabu yake ya Uholanzi ili apate baraka za Uhamisho.
Marco van Ginkel alijiunga na Vitesse
Arnhem akiwa na Miaka 7 tu na kupanda kwenye Vyuo vya Klabu hiyo hadi
Aprili 2010 alipocheza Timu ya Kwanza kwa mara ya kwanza.
Van Ginkel anathaminiwa kuwa na Dau la Pauni Milioni 8 na Mkataba wake na Klabu yake unamalizika Juni 2015.
Ikiwa Uhamisho huu utakamilika, huu
utakuwa ni usajili wa pili kwa Jose Mourinho baada ya Wiki iliyopita
kumnasa Mchezaji wa Kimataifa wa Germany, Andre Schurrle, kutoka Klabu
ya Bundesliga, Bayer Leverkusen.