Thursday, April 10, 2014

FIFA LISTI UBORA DUNIANI: SPAIN1, TANZANIA YA 122

Droo ya Listi ya ubora ya fifa  iliyotolewa Leo imeonyesha Mabingwa wa Dunia Spain bado wapo Nambari Wani wakifuatiwa na Germany, ambao wamebakia Namba 2, huku Tanzania ikiporomoka Nafasi 5 na kushika Nafasi ya 122 wakati Nafasi ya Juu kabisa kwa Nchi ya Afrika inakamatwa na Ivory Coast ambao wako Nafasi ya 21wakiwa wamepanda Nafasi 3.
FIFA_LOGOWenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia Mwaka huu, Brazil, wamepanda Nafasi 3 na sasa wapo Namba 6 pamoja na Argentina walioporomoka Nafasi 3.
Listi nyingine ya Ubora Duniani itatolewa tena na FIFA hapo Tarehe 8 Mei.
20 BORA DUNIANI:
1        Spain
2        Germany
3        Portugal       [Wamepanda Nafasi 1]
4        Colombia      [Wamepanda Nafasi 1]
5        Uruguay        [Wamepanda Nafasi 1]
6        Argentina     [Wameshuka Nafasi 3]
6        Brazil            [Wamepanda Nafasi 3]
8        Switzerland   [Wameshuka Nafasi 1]
9        Italy             [Wameshuka Nafasi 1]
10      Greece          [Wamepanda Nafasi 3]
11      England        [Wamepanda Nafasi 1]
12      Belgium        [Wameshuka Nafasi 2]
13      USA              [Wamepanda Nafasi 1]
14      Chile             [Wamepanda Nafasi 1]
15      Netherlands  [Wameshuka Nafasi 4]
16      France           [Wamepanda Nafasi 1]
17      Ukraine        [Wamepanda Nafasi 1]
18      Russia           [Wamepanda Nafasi 1]
19      Mexico          [Wamepanda Nafasi 1]
20      Croatia         [Wameshuka Nafasi 4]

UCL: BAYERN YAIPIGA MAN UNITED 3-1,BARCA NJE.

ROBO FAINALI
Marudiano
Jumatano Aprili 9
{Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili}
Bayern Munich 3 Manchester United 1 [4-2]
Atletico Madrid 1 Barcelona 0 [2-1]
Mabingwa Watetezi wa UCL, UEFA Championz Bayern Munich, jana Usiku wamefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Mashindano hayo baada ya kuitandika Manchester United goli 3-1 katika Mechi ya Marudiano ya Robo Fainali.
Katika Mtange wa Kwanza huko Old Trafford Wiki iliyopita, Timu hizi zilitoka Sare ya Bao 1-1.
Kwenye Mechi hii, Man United walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 57 la Patrice Evra lakini Bayern walijibu haraka na kusawazisha Dakika 2 baadae kwa Bao la Mario Mandzukic na kuongeza Bao mbili kupitia Thomas Muller, Dakika ya 68 na Arjen Robben, Dakika ya 76.
Bayern sasa wanaungana kwenye Nusu Fainali ya UCL pamoja na Chelsea, Atletico Madrid na Real Madrid.
Droo ya kupanga Mechi za Nusu Fainali itafanyika Ijumaa Aprili 11.
VIKOSI:
BAYERN MUNICH: Neuer, Dante, Ribery, Mandzukic, Robben, Boateng, Gotze, Lahm, Muller, Alaba, Kroos.
Akiba: Raeder, Van Buyten, Rafinha, Pizarro, Weiser, Hojbjerg, Weihrauch.
MAN UNITED: De Gea; Jones, Smalling, Vidic, Evra; Fletcher, Carrick; Valencia, Rooney, Kagawa; Welbeck.
Akiba: Lindegaard, Büttner, Ferdinand, Giggs, Januzaj, Young, Hernandez.
REFA: Jonas Eriksson [Sweden]
Goli la Dakika ya 5 la Koke limewapa ushindi Atletico Madrid wa Bao 1-0 dhidi ya Barcelona walipocheza Uwanjani kwao Estadio Vicente Calderon katika Mechi ya Marudiano ya Robo Fainali wa ligi ya mabingwa UCL,
katika mtanange wa awali timu hizi zilitoka Sare ya Bao 1-1 huko Nou Camp Wiki iliyopita.
Katika Mechi hiyo, Atletico walianza kwa kishindo na mbali ya kufunga Bao hilo mapema pia walipiga Posti mara 3 ndani ya Dakika 20 za kwanza.
Hii ni mara ya kwanza kwa Atletico kuingia Nusu Fainali ya Mashindano haya tangu Mwaka 1974 na ni mara ya kwanza kwa Barca kushindwa kuingia Nusu Fainali tangu 2007.
Msimu huu, Timu hizi zimekutana mara 4 na kutoka Sare.
Atletico sasa wanaungana kwenye Nusu Fainali ya UCL pamoja na Chelsea, Bayern Munich na Real Madrid.
Droo ya kupanga Mechi za Nusu Fainali itafanyika Ijumaa Aprili 11. 
VIKOSI:
Atletico Madrid: Courtois, Godin, Filipe Luis, Juanfran, Miranda, Tiago, Koke, Raul Garcia, Gabi, Adrian, Villa
Akiba: Aranzubia, Mario Suarez, Rodriguez, Alderweireld, Insua, Sosa, Diego.
Barcelona: Pinto, Mascherano, Bartra, Jordi Alba, Dani Alves, Fabregas, Xavi, Iniesta, Busquets, Messi, Neymar
Akiba: Oier, Montoya, Pedro, Alexis, Song, Adriano, Sergi Roberto.
REFA: Howard Webb [England]
UEFA CHAMPIONZ LIGI
ROBO FAINALI
Marudiano
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili]
Jumanne Aprili 8
Chelsea 2 Paris Saint-Germain 0 {3-3}, Chelsea wamesonga kwa Bao la Ugenini}
Borussia Dortmund 2 Real Madrid 0 {2-3}
DONDOO MUHIMU:
-DROO YA NUSU FAINALI: 11 Aprili
-Mechi kuchezwa 22 & 23 Aprili na Marudiano 29 & 30 Aprili
-FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014.
WASHINDI [Miaka ya karibu]:
MSIMU MSHINDI NCHI MSHINDI WA PILI NCHI GOLI
2012-13 Bayern Munich Germany Borussia Dortmund Germany 2-1
2011-12 Chelsea England Bayern Munich Germany 1-1 (4–3)
2010-11 Barcelona Spain Manchester United England 3-1
2009-10 Internazionale Italy Bayern Munich Germany 2-0
2008-09 Barcelona Spain Manchester United England 2-0
2007-08 Man United England Chelsea England 1-1 (6–5)

Wednesday, April 9, 2014

RUVU SHOOTING VS AZAM YAAHIRISHWA! YANGA YAPIGA 2-1 KAGERA KWA TABU.

VPL: LIGI KUU VODACOM
MATOKEO:
Jumatano Aprili 9
R/Shooting v Azam FC {Mechi imeahirishwa hadi alhamis aprili 10 mwaka huu}
Yanga 2 Kagera Sugar 1
MABINGWA Watetezi wa VPL, Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara, Wanajangwani Yanga sc, wakishuka katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam imefanikiwa kuibuka na ushindi ya kuinyuka Kagera Sugar Bao 2-1 na kujiwekea uimara katika mbio za kuwania ubingwa baada ya kujizatiti katika Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 1 nyuma ya Vinara Azam FC ambao Leo walishindwa kucheza Mechi yao kutokana na Mvua.
Hii Leo, Azam FC walikuwa wacheze huko Mabatini, Mlandizi dhidi ya Ruvu Shooting lakini Mechi hiyo ililazimika kuahirishwa kutokana na Mvua kubwa kufanya Uwanja ufurike maji.
Huku Timu zote zikiwepo Uwanjani, Waamuzi waliukagua Uwanja wa Mabatini na kujiridhisha kuwa haufai kuchezwa na ndipo wakaamua kuahirisha Mechi hiyo.
Habari za awali zimesema kuwa Mechi hii itachezwa kesho.
Huko Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga waliifunga Kagera Sugar Bao 2-1 kwa Bao za Kipindi cha Kwanza zikifungwa na Hamisi Kiiza, Dakika ya 3, na Didier Kavumbagu, Dakika ya 34 wakati Kagera Sugar walifunga Bao lao Dakika ya 63 kupitia Daud Jumanne.
Yanga, ambao wako Pointi 1 nyuma ya Vinara Azam FC, sasa wamebakisha Mechi mbili dhidi ya JKT Oljoro, huko Arusha, na Simba wakati Azam FC wana Mechi 3 dhidi Ruvu Shooting, Mbeya City huko Mbeya na JKT Ruvu.
RATIBA:
Jumamosi Aprili 12
Mtibwa Sugar vs Ruvu Shooting (Manungu, Morogoro),
Coastal Union vs JKT Ruvu (Mkwakwani, Tanga),
Tanzania Prisons vs Rhino Rangers (Sokoine, Mbeya).
Jumapili Aprili 13
Mgambo Shooting vs Kagera Sugar (Mkwakwani, Tanga),
Simba vs Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam)
Mbeya City vs Azam (Sokoine, Mbeya)
JKT Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
GF
PTS
1
Azam FC
23
15
8
0
31
45
53
2
Yanga SC
24
15
7
2
41
58
52
3
Mbeya City
24
12
10
2
13
30
46
4
Simba SC
24
9
10
5
15
40
37
5
Kagera Sugar
24
8
10
6
2
22
34
6
Ruvu Shooting
22
9
7
6
0
27
34
7
Mtibwa Sugar
25
7
10
8
0
28
31
8
Coastal Union
24
6
11
7
-2
16
29
9
JKT Ruvu
23
8
1
14
-19
19
25
10
Mgambo Shooting
23
6
6
11
-16
16
24
11
Ashanti UTD
23
4
7
12
-20
17
19
12
JKT Oljoro
24
3
9
12
-17
17
18
13
Prisons FC
22
3
9
10
-11
17
18
14
Rhino Rangers
23
3
7
13
-17
15
16

UCL:CHELSEA YAIPAPATUA PSG 2-0 YACHUPA NUSU FAINALI.

Matokeo Marudio.
Jumanne Aprili 8
aprilChelsea 2 Paris Saint-Germain 0 [3-3, Chelsea wamesonga kwa Bao la Ugenini]
Borussia Dortmund 2 Real Madrid 0 [2-3]
CHELSEA FC 2 PARIS SAINT-GERMAIN 0
-Stamford Bridge, London
Club ya Chelsea imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL baada ya Bao la Demba Ba la Dakika ya 87 kuwapa ushindi wa Bao 2-0 katika Mechi ya Marudiano iliyochezwa Stamford Bridge na kufanya Jumla ya Mabao kuwa Bao 3-3 katika Mechi mbili na wao kutinga hatua inayofuata ya Nusu fainali kwa  Bao la Ugenini.
Bao la Kwanza la Chelsea lilifungwa na Andre Schurrle, alieingizwa kumbadili Eden Hazard alieumia, katika Dakika ya 32.
Demba Ba ambae alitokea Benchi na Bao lake la ushindi kwa Chelsea lilimfanya Meneja wao Jose Mourinho ashangilie kwa aina ya kipekee.
VIKOSI:
CHELSEA: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Luiz, Lampard, Willian, Oscar, Hazard, Eto'o.
Akiba: Schwarzer, Cole, Kalas, Mikel, Schurrle, Ba, Torres.
PSG: Sirigu, Jallet, Alex, Silva, Maxwell, Verratti, Motta, Matuidi, Lucas, Cavani, Lavezzi.
Akiba: Douchez, Marquinhos, Digne, Van der Wiel, Cabaye, Menez, Pastore.
REFA: Pedro Proença (Portugal) 

UEFA CHAMPIONZ LIGI
ROBO FAINALI
Marudiano
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Jumatano Aprili 9
Bayern Munich v Manchester United [1-1]
Atletico Madrid v Barcelona [1-1]
DONDOO MUHIMU:
-DROO YA NUSU FAINALI: 11 Aprili
-Mechi kuchezwa 22 & 23 Aprili na Marudiano 29 & 30 Aprili
-FAINALI: Estádio da Luz, Lisbon, Portugal 24 Mei 2014.
WASHINDI [Miaka ya karibu]:
MSIMU MSHINDI NCHI MSHINDI WA PILI NCHI GOLI
2012-13 Bayern Munich Germany Borussia Dortmund Germany 2-1
2011-12 Chelsea England Bayern Munich Germany 1-1 (4–3)
2010-11 Barcelona Spain Manchester United England 3-1
2009-10 Internazionale Italy Bayern Munich Germany 2-0
2008-09 Barcelona Spain Manchester United England 2-0
2007-08 Man United England Chelsea
England
1-1 (6–5)

Tuesday, April 8, 2014

VPL: AZAM VS RUVU SHOOTING MLANDIZI,YANGA VS KAGERA SUGAR U/TAIFA.

TIMU TATU FDL ZARUDI LIGI YA MKOA
Timu tatu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zitacheza Ligi ya Mkoa katika mikoa yao msimu ujao baada ya kushika nafasi za mwisho katika makundi yao, hivyo kushuka daraja.

Transit Camp imekata nafasi ya mwisho katika A wakati Mkamba Rangers imeshuka daraja kwa kukamata mkia katika kundi B. Nayo Pamba SC imerudi kucheza Ligi ya Mkoa wa Mwanza baada ya kuwa ya mwisho kwenye kundi C.
Timu zilizopanda daraja kutoka FDL kwenda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao ni Ndanda SC ya Mtwara kutoka kundi A, Polisi Morogoro ya kundi B na Stand United ya Shinyanga iliyoibuka kinara katika kundi C.

AZAM, YANGA KUTIMULIANA VUMBI VPL
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Aprili 9 mwaka huu) huku timu za Azam na Yanga ambazo zipo nafasi mbili za juu zikiendelea kuchuana.

Azam itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting katika mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani. Nayo Yanga itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar katika Uwanja wa Taifa jijini.

Yanga, Azam, Ruvu Shooting na Kagera Sugar zote zimeshinda mechi zao za raundi ya 23 wakati mechi za kesho zitakuwa kwa ajili ya kukamilisha raundi ya 24 ya ligi hiyo ambayo inatarajia kukamilika Aprili 19 mwaka huu.

Ligi hiyo itaingia raundi ya 25 Aprili 12 na 13 mwaka huu ambapo timu zote 14 zitakuwa viwanjani. Aprili 12 mwaka huu itakuwa Mtibwa Sugar vs Ruvu Shooting (Manungu, Morogoro), Coastal Union vs JKT Ruvu (Mkwakwani, Tanga), na Tanzania Prisons vs Rhino Rangers (Sokoine, Mbeya).

Aprili 13 mwaka huu ni Mgambo Shooting vs Kagera Sugar (Mkwakwani, Tanga), Simba vs Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Mbeya City vs Azam (Sokoine, Mbeya) na Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).

TFF YAAFIKA UAMUZI WA KAMATI YA MAADILI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekubaliana na uamuzi uliofanywa na Kamati ya Maadili katika malalamiko mawili ambayo iliyawasilisha mbele yake, hivyo haitakata rufani.

Katibu Mkuu wa TFF aliwasilisha mashauri mawili mbele ya Kamati hiyo iliyoongozwa na William Erio. Malalamiko ya kwanza yalikuwa dhidi ya waamuzi wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Oden Mbaga na Samwel Mpenzu na wakufunzi wa waamuzi Riziki Majala na Mchungaji Army Sentimea.

Wote aliwalalamikia kwa kuwafanyisha mitihani (wakufunzi), na waamuzi kufanya mitihani hiyo kinyume na utaratibu pamoja na kughushi matokeo.

Kamati katika uamuzi wake iliiagiza waamuzi hao kufanya upya mtihani huo katika robo inayofuata ambapo wakifaulu waendelee kuchezesha mechi. Waamuzi wa FIFA hufanya mitihani hiyo mara nne kwa mwaka.

Kwa upande wa shauri dhidi ya Ofisa Takwimu wa TFF, Sabri Mtulla ambaye alilalamikiwa kwa kuidanganya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuwa hakukuwa na pingamizi dhidi ya mchezaji Emmanuel Okwi, Kamati iliagiza suala hilo liwasilishwe upya pamoja na ushahidi wa kuthibitisha malalamiko hayo.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Monday, April 7, 2014

NGORONGORO HEROES KUINGIA KAMBINI ALHAMISI

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngongoro Heroes) imereja nchini leo mchana (Aprili 7 mwaka huu) kutoka Kenya mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya wenyewe, na itaingia kambini Alhamisi.
Ngorongoro Heroes ambayo imewasili saa 8.25 kwa ndege ya Kenya Airways ilitoka suluhu na Kenya katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Kanyetta uliopo katika mji wa Machakos.
Kocha John Simkoko amesema benchi lake la ufundi linafanyika kazi upunguzi uliojitokeza ili wafanye vizuri kwenye mechi ya marudiano itakayochezwa Aprili 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Iwapo Ngorongoro Heroes itaitoa Kenya, raundi inayofuata itacheza na Afrika Kusini. Fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 zitafanyika mwakani nchini Senegal.