MSIMU wa VPL Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara umefikia tamatu jumamosi ya aprili 19 mwaka huu kwa Azam FC kutawazwa kuwa mabingwa wapya baada ya
kumaliza na pointi 62 dhidi ya 56 za waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga SC
baada ya mechi zote 26.
Licha
ya kuwa timu ya kwanza kuifunga Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine Aprili 13,
mwaka huu,
Azam FC pia inakuwa timu ya kwanza nje ya Simba na Yanga kutwaa
ubingwa wa Bara tangu mwaka 2000 Mtibwa Sugar ilipofanya hivyo
Azam inakuwa timu ya saba nje ya
Si
mba SC kutwaa taji la Ligi Kuu, baada ya Cosmo mwaka 1967, Mseto mwaka 1975,
Pan Africans mwaka 1982, Tukuyu Stars mwaka 1986, Coastal Union 1988 na Mtibwa
Sugar mara mbili mfululizo 1999 na 2000.

Ashanti United ya Ilala, Dar es
Salaam inayomaliza ligi na pointi 25, inaungana na JKT Oljoro ya Arusha
iliyomaliza na pointi 19 na Rhino Rangers ya Tabora pointi 16 kuipa mkono wa
kwaheri Ligi Kuu msimu wa 2013/2014 na nafasi zao kuchukuliwa na Ndanda FC ya
Mtwara, Polisi ya Morogoro na Stand United ya Shinyanga zilizopanda kwa ajili
ya msimu ujao.
Mbali na Azam kumaliza kileleni na
pointi 62, Yanga SC pointi 56 nafasi ya pili, Mbeya City ya Mbeya imemaliza
nafasi ya tatu kwa pointi zake 49, Simba SC ya nne pointi 38, Kagera Sugar ya
tano pointi 38 pia, Ruvu Shooting ya sita pointi 38, Mtibwa Sugar ya saba
pointi 31, JKT Ruvu ya nane pointi 31 Coastal Union ya tisa pointi 29, Prisons
ya 10 pointi 28 na JKT Mgambo ya 11 pointi 26.
Huku tunahitimisha pazia la Ligi Kuu
pamoja na kufurahia kufika salama, lakini ukweli ni kwamba kuna mapungufu mengi
yaliyojitokeza ndani ya msimu huu ambayo yangeweza hata kusababisha athari
kubwa.

Miongoni
mwa hayo ni suala la uchezeshaji wa marefa, mfumo na muundo mzima wa ligi yetu
ikiwa ni pamoja na kanuni kutozingatiwa, au kuwa na kanuni ambazo hazikidhi
vigezo vya kimataifa.
Kanuni ya tano ya Ligi Kuu inasema
kifungu cha (1) Uwanja wa nyumbani ni ule ul
iochaguliwa na timu husika na
Uwanja wa ugenini ni ule ambao timu pinzani imekaribishwa kucheza.
Kifungu
cha (2) Kutokana sababu za kiusalama au Uwanja, kutofikika au sababu nyingine
yeyote ya msingi, TFF kwa kushauriana na timu husika, endapo timu yoyote haina
Uwanja wa nyumbani unaofaa kwa mashindano ya Ligi, timu husika inaweza kuchagua
kwa idhini ya TFF, Uwanja mwingine wowote, hata nje ya mji huo au Mkoa ili
mradi Uwanja huo uwe jirani na mkoa wa timu husika ndani ya Tanzania Bara na
uwe na sifa zinazokubalika,”.
Kuna tatizo katika kanuni hii,
ukipitia kanuni nyingine nyingi duniani, zinaweka wazi kwamba timu itakuwa na
Uwanja mmoja tu wa nyumbani, lakini kanuni hii ya ligi yetu imefumbwa na
matokeo yake timu kama Ruvu Shooting, Mtibwa Sugar Azam FC na Prisons msimu huu
zimetumia Uwanja zaidi ya mmoja wa nyumbani.
Ruvu, Mtibwa na Azam zimeruhusiwa
kutumia viwanja vyao kwa mechi zote za Ligi Kuu isipokuwa zile zinazohusu Simba
na Yanga, kwa sababu timu zote za Kariakoo, Dar es Salaam zina mashabiki wengi.