Saturday, January 3, 2015

MAPINDUZI CUP: YANGA SC YAUWA MSUVA NYOTA YAZIDI KUPETA HETITRIKI!

Watoto wa Jangwani Yanga Sc imeanza vyema kwa kishindo cha aina yake katika Mashindano ya Mapinduzi Cup 2015 huko Visiwani Zanzibar walipoichapa Taifa ya Jang’ombe ya Zanzibar Bao 4-0 katika Mechi ya Kundi A huku Simon Msuva akipiga Bao 3.
Bao jingine la Yanga lilifungwa na Kpah Sherman kutoka Liberia.
Katika Mechi zilizotangulia hii Leo, KMKM na Mtende zilitoka 0-0 na Azam FC kutoka pia Sare ya 2-2 na Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, KCCA ya Uganda.
MAKUNDI
KUNDI A
-Yanga
-Taifa ya Jang’ombe [Zanzibar]
-Shaba [Pemba]
-Polisi [Zanzibar]
KUNDI B
-KCCA [Uganda]
-Azam FC
-KMKM [Zanzibar]
-Mtende [Zanzibar]
KUNDI C
-Simba
-Mtibwa Sugar
-JKU [Zanzibar]
-Mafunzo [Zanzibar]
RATIBA/MATOKEO:
Saa za Bongo
Mechi zote kuchezwa Uwanja wa Amaan isipokuwa inapotajwa
Alhamisi Januari 1
JKU 2 Mafunzo 0
Polisi 1 Shaba 0
Simba 0 Mtibwa 1
Ijumaa Januari 2
KMKM 0 Mtende 0
KCCA 2 Azam FC 2
Yanga 4 Taifa ya Jang’ombe 0
Jumamosi Januari 3
3:00 JKU v Mtibwa
5:00 Mafunzo v Simba
Jumapili Januari 4
1500 KCCA v Mtende
1700 KMKM v Azam FC
1500 Taifa ya Jang’ombe v Shaba [Uwanja wa Mao]
2015 Yanga v Polisi
Jumatatu Januari 5
1500 Mtibwa v Mafunzo
2015 Simba v JKU
Jumanne Januari 6
1500 KCCA v KMKM
1500 Polisi v Taifa ya Jang’ombe [Uwanja wa Mao]
1700 Azam FC v Mtende
2015 Yanga v Shaba
Jumatano Januari 7
Robo Fainali
Mshindi Kundi C v Mshindi wa 3 Bora Na. 2
Mshindi wa Pili Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi C
Alhamisi Januari 8
Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A
Mshindi Kundi A v Mshindi wa 3 Bora Na. 1
Jumamosi Januari 10
Nusu Fainali
Mshindi RF 1 v Mshindi RF 2
Mshindi RF 3 v Mshindi RF 4
Jumanne Januari 13
Fainali

Tuesday, December 30, 2014

AZAM, MTIBWA, SIMBA, YANGA KUCHEZA MAPINDUZI HIVYO BASI MECHI ZAO ZAPIGWA KALENDA

Timu za Azam, Mtibwa Sugar, Simba na Yanga zitashiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayofanyika kisiwani Zanzibar kuanzia Januari 1 hadi 13 mwakani.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ruhusa kwa timu hizo kucheza mashindano hayo baada ya kuhakikishiwa na Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kuwa kesi iliyofunguliwa dhidi ya viongozi wake imeondolewa mahakamani.
Kutokana na timu hizo kushiriki Kombe la Mapinduzi, mechi zao za raundi ya tisa na kumi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitachezwa katikati ya wiki baada ya kumaliza mechi zao za michuano hiyo.
Hivyo mechi za VPL ambazo hazitachezwa wikiendi hii ni kati ya Azam na Mtibwa Sugar, Mbeya City na Yanga, na ile kati ya Mgambo Shooting na Simba. Mechi za wikiendi ijayo zinazopisha michuano hiyo ni kati ya Kagera Sugar na Azam, Coastal Union na Yanga, Mbeya City na Simba, na Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons.

18 WAPATA BEJI ZA UAMUZI FIFA
Waamuzi 18 wa Tanzania wamepata beji za uamuzi za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa mwaka 2015.
Idadi hiyo ambayo ni rekodi kwa Tanzania inahusisha waamuzi saba wa kike. Waamuzi wa kati wa kike waliopata beji hizo ni pamoja na Jonesia Rukyaa Kabakama aliyechezesha mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga. Wengine ni Florentina Zablon Chief na Sophia Ismail Mtongori.
Waamuzi wasaidizi wa kike waliopata beji hizo ni Dalila Jafari Mtwana, Grace Wamala, Hellen Joseph Mduma na Kudura Omary Maurice.
Kwa waamuzi wa kati wa kiume ni Israel Mujuni Nkongo, Martin Eliphas Sanya, Mfaume Ali Nassoro na Waziri Sheha Waziri. Waamuzi wasaidizi ni Alli Kinduli, Ferdinand Chacha, Frank John Komba, John Longino Kanyenye, Josephat Deu Bulali, Samuel Hudsin Mpenzu na Soud Iddi Lila.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Sunday, December 28, 2014

LIGI KUU YA VODACOM YAINGIA RAUNDI YA 9 MWAKANI 2015 JANUARY 3 NA 4 VIWANJA MBALIMBALI NCHINI

Wakati raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inakamilika leo (Desemba 29 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo yanga iliumana na azam fc na kutoka sare ya 2-2 na mbeya city ikiichapa ndanda fc 1-0 huku polisi moro ikiichaklza Jkt Mgambo 1-0 Huku Matokeo ya jana Prison ikitoka sare na Costal Union 0-0.
Ligi hiyo itaingia raundi ya tisa Januari 3 mwakani kwa mechi tano Coastal Union itacheza na JKT Ruvu katika Uwanja wa Mkwakwani, Ruvu Shooting itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Azam itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Azam Complex, Stand United itakuwa mgeni wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri wakati Mbeya City na Yanga zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Sokoine.
Ligi hiyo ambayo itachezwa mfululizo (non-stop) hadi itakapomalizika Mei 9 mwakani, itakamilisha raundi ya tisa Januari 4 mwakani kwa mechi kati ya Mgambo Shooting na Simba kwenye Uwanja wa Mkwakwani, na Tanzania Prisons itakayokuwa mwenyeji wa Ndanda kwenye Uwanja wa Sokoine.
Nayo mechi kati ya Mtibwa Sugar na Stand United ambayo jana ilivunjwa na mvua dakika ya 6 imemaliziwa leo ambapo timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1.
Wakati huo huo, mechi ya ligi iliyochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex imemalizika kwa wageni Ruvu Shooting kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu. Bao hilo lilifungwa kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Hamisi Kasanga.  
MSIMAMO VPL LIGI KUU TANZANIA BARA:

NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Mtibwa Sugar
8
4
4
0
11
4
7
16
2
Yanga
8
4
2
2
11
6
4
14
3
Azam FC
8
4
2
2
10
6
4
14
4
Kagera Sugar
8
3
4
1
6
3
3
13
5
Coastal Union
8
3
3
2
8
6
2
12
6
JKT Ruvu
8
3
1
4
7
8
-1
10
7
Ruvu Shooting
8
3
1
4
5
7
-2
10
8
Stand United
8
2
4
2
6
10
-4
10
9
Simba
8
1
6
1
7
7
0
9
10
Polisi Moro
7
3
2
2
6
7
-1
9
11
Mgambo JKT
7
3
0
4
4
7
-3
9
12
Mbeya City
8
2
2
4
4
5
-1
8
13
Tanzania Prisons
8
1
4
3
5
6
-1
7
14
Ndanda FC
8
2
0
6
8
13
-5
6

TIMU YA MBAO FC YAKAMATA USUKANI LIGI DARAJA LA PILI{SDL}
Timu ya Mbao FC ya Mwanza imekamata uongozi wa Kundi B la michuano ya Ligi Daraja la Pili (SDL) baada ya jana (Desemba 27 mwaka huu) kuizamisha JKT Rwamkoma ya Mara mabao 2-1.
Kwa matokeo hayo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mbao FC imeitoa kileleni JKT Rwamkoma baada ya kufikisha pointi tisa kwa kushinda mechi zote tatu dhidi ya Arusha FC, Pamba na JKT Rwamkoma.
Mbao FC inafuatiwa na JKT Rwamkoma yenye pointi sita, Arusha FC pointi sita wakati Bulyanhulu na Pamba zikiwa za mwisho kwa pointi moja kila moja. Kundi hilo litakamilisha mzunguko wa kwanza Januari 3 mwakani kwa mechi kati ya JKT Rwamkoma na Arusha FC, na Bulyanhulu na Mbao FC.
Katika kundi A, Mji Mkuu (CDA) na Singida United ndizo zinazochuana kileleni kwa kufikisha pointi saba kila moja. Timu hizo zinafuatiwa na Milambo yenye pointi nne, Mvuvumwa FC yenye pointi moja wakati Ujenzi Rukwa ni ya mwisho ikiwa haina pointi.
Hata hivyo, Mvuvumwa FC na Milambo ziko nyuma kwa mechi moja. Mechi hiyo ya kukamilisha raundi ya tatu kati ya timu hizo itachezwa kesho (Desemba 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Kiluvya United imeendelea kuchachafya kundi C baada ya kushinda mechi zote ne ilizocheza, hivyo kufikisha pointi 12. Inafuatiwa na Mshikamano yenye pointi saba huku Abajalo ikiwa katika nafasi ya tatu kwa pointi 6.
Nafasi ya nne inashikwa na Transit Camp yenye pointi nne, Cosmopolitan yenye pointi mbili ni ya tano wakati Kariakoo ambayo haina pointi ni ya mwisho. Hata hivyo, Cosmopolitan na Kariakoo zina mchezo mmoja mkononi.
Mechi zinazofuata za kundi hilo ni Januari 3 mwakani kati ya Kariakoo na Mshikamano na Mshikamano (Ilulu), Transit Camp na Abajalo (Mabatini), na Cosmopolitan na Kiluvya (Karume).
Kundi D, vinara bado ni Njombe Mji yenye pointi 12 ikifuatiwa na Wenda yenye pointi sita wakati Volcano FC iko nafasi ya tatu ikiwa na pointi tano. Mkamba Rangers ina pointi nne, Town Small Boys ina pointi moja wakati Magereza FC haina pointi.
Katika kundi hilo leo (Desemba 28 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Town Small Boys na Magereza itakayochezwa Uwanja wa Majimaji mjini Songea.  Januari 3 mwakani kutakuwa na mechi kati ya Town Small Boys na Njombe Mji, Volcano FC na Magereza, na Wenda na Mkamba Rangers.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)