Sunday, May 12, 2013

AZAM FC YAITANDIKA JKT MGAMO 3-0 KUCHEZA KOMBE LA SHIRIKISHO

AZAM FC imefanikiwa rasmi kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Mgambo Shooting jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Ushindi huo, unaifanya Azam ifikishe pointi 51, nne nyuma ya mabingwa, Yanga SC wenye 57 kila timu ikiwa imebakiza mechi moja kumaliza ligi.

Hadi mapumziko, tayari Azam FC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na John Raphael Bocco dakika ya 23 kufuatia kazi nzuri9 ya Humphrey Ochieng Mieno.
Kipindi cha pili, Azam tena walirudi na kasi nzuri na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 65 lililofungwa na Kipre Herman Tchetche baada ya kuichambua ngome ya wapinzani na kupioga shuti mariadi.
Hilo lilikuwa bao lake la 17 msimu huu hivyo kujihakikishia ufungaji bora wa Ligi Kuu, akiritihi mikoba ya Bocco ‘Adebayor’, ambaye naye alimrithi Mrisho Khalfan Ngassa akiwa Azam pia kabla ya kutolewa kwa mkopo Simba SC.  
Joackins Otieno Atudo aliunganishwa kwa kichwa kona ya Erasto Edward Nyoni dakika ya 80 na mpira ukatinga nyavuni na hata kipa Tonny Kavishe alipojaribu kuuokolea ndani, lakini ukagonga nyavu za juu na kudondokea ndani tena, hilo likiwa bao la tatu katika mchezo wa leo.
Azam sasa watacheza tena michuano ya Shirikisho mwakani, baada ya mwaka huu kutolewa Raundi ya Tatu na AS FAR Rabat ya Morocco wakishiriki kwa mara ya kwanza.

VIKOSI VYA TIMU ZOTE MBILI
Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Aggrey Morris, Joackins Atudo, Kipre Balou/Ibrahim Mwaipopo dk85, Kipre Tchetche, Salum Abubakar, John Bocco, Humprey Mieno/Abdi Kassim dk83 na Brian Umony/Seif Abdallah dk63. 
JKT Mgambo; Tony Kavishe, Salum Mlima, Ramadhani Malima, Bashiru Chanacha, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Mussa Gunda, Juma Mwinyimvua/Peter Mwalyanzi dk 56, Issa Kandulu, Fully Maganga na Nassor 
Gumbo.

 RATIBA.
Jumamosi Mei 18
Toto Africans Vs Ruvu Shooting
Mgambo JKT Vs African Lyon
JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar
TZ Prisons Vs Kagera Sugar
Simba SC Vs Yanga SC
JKT Oljoro Vs Azam FC
Polisi Moro Vs Coastal Union
MSIMAMO:
KUMBUKA YANGA BINGWA
NA
TIMU
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
YANGA
25
17
6
2
45
14
31
57
2
AZAM FC
25
14
6
4
42
20
25
51
3
SIMBA SC
25
12
9
4
38
23
15
45
4
KAGERA SUGAR
25
11
7
6
25
18
8
41
5
MTIBWA SUGAR
25
10
9
6
29
24
5
39
6
COASTAL UNION
25
8
11
6
25
23
2
35
7
RUVU SHOOTING
25
8
7
9
21
23
-2
32
8
JKT OLJORO
25
7
8
10
21
26
-5
29
9
TANZANIA PRISONS
25
7
8
10
16
22
-6
29
10
JKT RUVU
25
7
5
13
21
38
-17
26
11
MGAMBO SHOOTING
25
7
4
13
16
24
-8
25
12
POLISI MOROGORO
25
4
10
11
13
23
-10
22
13
TOTO AFRICAN
25
4
10
11
21
33
-12
22
14
AFRICAN LYON
25
5
4
16
16
38
-22     
19