Sunday, May 19, 2013

ROY AKERWA NA CHELSEA, MAN CITY VS TOTTENHAM KWENA MAREKANI.

Meneja wa England ROY HODGSON amekerwa na kitendo cha uamuzi wa Klabu za Chelsea, Manchester City na Tottenham kusafiri kwenda ya nje ya Nchi kucheza Michezo ya Kirafiki wakati ndio kwanza Msimu umemalizika.

Klabu hizi 3 zitasafiri n kuelekea Marekani kuumana  zenyewe kwa wenyewe katika Mechimbili za kirafiki huku Tottenham wakitua Visiwa vya Bahamas kucheza na Jamaica.
ZIARA:
Mei 23: Man City v Chelsea [St Louis]
Mei 25: Chelsea v Man City [New York]
Mei 23: Tottenham v Jamaica [Thomas A. Robinson National Stadium, Nassau Paradise Island, Bahamas]
England nayo inatarajiwa kucheza na Republic of Ireland, Uwanjani Wembley hapo Mei 29 na kisha kuruka kwenda Brazil kucheza Uwanja wa Maracana Jijini Rio De Janeiro na Brazil hapo Juni 2.
Kikosi cha Hodgson alichokiteua kuiwakilisha England katika Mechi hizo mbili kina Wachezaji wanane toka Timu hizo tatu.
Chelsea inasemekana imekubali kuwaruhusu Frank Lampard, Ashley Cole na Gary Cahill kuondoka baada ya Mechi yao ya kwanza ya Tarehe 23 na Man City ili kurudi London kujiunga na England.
Lakini Hodgson amesema wao walipanga Mechi zao za Kimataifa kwa makusudi ili kuwapa Wachezaji wote mapumziko ya Wiki moja baada ya Msimu wa Klabu zao kumalizika kisha kuwachukua wao kwa Wiki moja na baada ya hapo kuwaachia kwenda Vakesheni zao kabla kurudi Klabuni kwao kwa matayarisho ya Msimu mpya wa 2013/14.
Hogson amesema Ziara hizo za Klabu zitawafanya wasafiri safari ndefu kuvuka Bahari ya Atlantic na kurudi tena na hilo halitasaidia matayarisho yao.
Akimalizia Hodgson alisema: “Hii ndio hali ambayo tumejikuta tunayo na hatuwezi kulazimisha Klabu nini wafanye.”
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Ben Foster, Joe Hart, Alex McCarthy.
MABEKI: Leighton Baines, Gary Cahill, Ashley Cole, Phil Jagielka, Glen Johnson, Phil Jones, Joleon Lescott, Kyle Walker.
VIUNGO: Michael Carrick, Tom Cleverley, Frank Lampard, James Milner, Alex Oxlade-Chamberlain, Theo Walcott.
MAFOWADI: Andy Carroll, Jermain Defoe, Wayne Rooney, Daniel Sturridge, Danny Welbeck.