Wakisheherekea ubingwa wao Timu ya Manchester United huku ikimuaga kwa kila heri Meneja wao Sir Alex Ferguson baada ya Miaka 26 ya Utumishi uliojawa na furaha tele kwa Jumapili walikabidhiwa Kombe la Ubingwa England na Jumatatu Jioni wakizunguuka nalo Mitaa ya Jiji hilo kwa Maandamano ya furaha kubw lakini upande wa pili wa Manchester City mekuwa na majonzi makubwa baada ya kuukosa Ubingwa na Juzi kukosa FA CUP walitandikwa na Wigan kwenye Fainali, na hili leo kilio chao kuhitimishwa kwa Meneja wao Roberto Mancini kutupiliwa virago katika timu hiyo.
kitu kilichopelekea kutimuliwa kazi kwa Roberto Mancini alidumu kwa Miaka mitatu na nus, tamko la Klabu lisema: manchin Ameshindwa kutimiza malengo ya Klabu Msimu huu ukiachia kufuzu kucheza UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
Klabu hiyo imesema Meneja Msaidizi, Brian Kidd, ambae alishawahi kuwa Msaidizi wa Sir Alex Ferguson huko Man United, ndio atakaimu nafasi hiyo kwa Mechi zao mbili za BPL zilizobaki za Msimu huu na pamoja na Ziara yao ya kabla ya Msimu mpya kuanza ya huko Marekani.

Mara baada kufungwa na Wigan kwenye FA CUP, Mancini alikurupuka na kuulaumu uongozi wa Man City kwa kutokanusha uvumi wa Pellegrini, Raia wa Chile, kuja kutwaa kazi yake.
hata hivyo ingawa Mancini aliiwekea Man City historia nzuri ya kutwaa Kombe lao la kwanza baada ya
Miaka 35 walipotwaa FA CUP na kutwaa Ubingwa wao wa kwanza baada ya Miaka 44, kumaliza Msimu huu kwa ukame kunadaiwa kuwakera Wamiliki Matajiri wa Man City toka Falme za Nchi za Kiarabu ambao Jumamosi walikuwa Wembley kushuhudia Timu yao ikitwaa Kombe kwa mgongo wa ‘vibonde’ Wigan lakini wakajikuta chali baada ya kutunguliwa Bao 1-0 na Kombe la FA CUP kwenda Wigan, Timu ambayo huenda Msimu huu ikaandika Historia ya kuwa Klabu ya kwanza kutwaa FA CUP na kushushwa toka Ligi Kuu Msimu huo huo.
Kocha ambaye anatarajiwa kuchukuwa mikoba ya manchin ni Manuel Pellegrini, Kocha wa Malaga ya Spain raia wa Chile, atapewa wadhifa wa kumrithi Mancini ingawa mwenyewe amesisitiza hayo si kweli.