
MSHAMBULIAJI nyota mpya wa Fc Barcelona,Neymar jana alifanikiwa kung'arisha nyota yake katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mabara, akifunga bao la mapema dakika ya tatu wakati Brazil inailaza 3-0 Japan.
Mshambuliaj huyo nyota wa Brazil, alifunga kwa shuti la nje ya eneo la hatari, akiunganisha pasi ya Fred ambaye naye alipokea krosi ya Marcelo kwa kifua kwanza.
Ushindi huo unaiweka Brazil kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake tatu. Italia na Mexico watamenyana leo katika mechi nyingine ya kundi hilo.
Kikosi cha Brazil jana kilikuwa; Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Oscar, Gustavo, Paulinho, Fred/Jo dk81, Neymar/Lucas Moura dk74 na Hulk/Hernanes dk75.
Japan: Kawashima, Konno, Nagatomo, Uchida, Yoshida, Endo/Hosogai dk77, Honda/Inui dk88, Kiyotake/Maeda dk51,Kagawa, Hasebe na Okazaki.