SHIRIKISHO la Soka
Duniani-FIFA linafuatilia kwa karibu kashfa ya upangaji matokeo
inayozikabili vilabu viwili vya soka vya ridhaa nchini Nigeria
iliyotokea wiki iliyopita. Katika
matokeo ambayo yanaonekana kama ya mchezo wa kriketi, klabu ya Plateau
United Feeders iliibugiza Akurba FC kwa mabao 79-0 wakati Police Machine
wao waliitandika Bubayaro FC kwa mabao 67-0 mwishoni mwa wiki
iliyopita. Hatua uchunguzi kwa vilabu hivyo imekuja kutokana na timu hizo kuhitaji matokeo ya aina hiyo ili waweze kupanda daraja. Ambapo
katika taarifa yake FIFA imedai kuwa inafuatilia tukio hilo la tmu hizo
za Nigeria kwa karibu ili kuona jinsi gani Shirikisho la Soka la nchi
hiyo, NFF litatatua tatizo hilo. FIFA
inafanya hivyo kwa kutambua kuwa suala hilo ni la ndani hivyo NFF ina
wajibu wa kufanya uchunguzi na kuchukua hatua zinazostahiki kama
ikigundulika aina yoyote ya udanganyifu katika mechi hizo.