KAMPUNI YA MADUKA NCHINI BRAZIL WATISHIA KWENDA MAHAKANI KUHUSU USAJILI NEYMAR
Kampuni ya DIS
inayomiliki maduka makubwa nchini Brazil na ambao wanamiliki asilimia 40
ya haki za usajili wa Neymar wametishia kwenda mahakamani kuhusiana na
mgao wao kwa nyota huyaa o katika usajili wake kwenda Barcelona. Kampuni
hiyo inayoendeshwa na Idi Sonda imedai kuwa na haki ya kupata fedha
zaidi juu ya makubaliano ya ziada kati ya klabu ya Santos na Barcelona
ambayo yako nje ya ada ya uhamisho wake ambayo ilifikia kiasi cha euro
milioni 57. Mkurugenzi
Mtendaji wa DIS, Roberto Moreno ameomba kupewa taarifa kamili ya hati
ya uhamisho wa Neymar kwenda Barcelona ili kupata ufafanuzi kuhusu
malipo ya baadae watakayopewa Santos. Moreno
amesema mpaka kipindi hicho hawajaonyeshwa hati yoyote, hivyo atafunga
safari kwenda makao makuu ya Santos kufuatilia hati hiyo na baada ya
hapo wataamua kama watahitaji kwenda mahamani. Hatua
ya kampuni hiyo imekuja kufuatia taarifa zilitolewa na vyombo vya
habari nchini humo kwamba Santos watapata nyongeza ya euro milioni mbili
kama mchezaji huyo atakuwemo katika orodha ya wachezaji watatu kwenye
tuzo ya Ballon d’Or kwenye kipindi cha miaka mitano ijayo.