Marion Bartoli mwanadada nyota katika
tenisi, amefanikiwa kushinda taji lake la kwanza la
michuano ya Grand Slam baada ya kumchalaza Sabine Lisicki wa Ujerumani
kwa seti 6-1 6-4 kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Wimbledon. Bartoli
ambaye anashika namba 15 katika orodha za ubora kwa upande wanawake
alitumia dakika 30 pekee kushinda seti ya kwanza wakati mpinzani wake
Lisicki akionekana kushindwa kumudu vishindo katika fainali yake ya
kwanza ya Grand Slam. Akihojiwa
mara baada ya mchezo huo Bartoli amesema haamini kama amenyakuwa taji
hilo na alikuwa akijisikia kucheza kwa kiwango chake cha juu huku kila
kitu alichofanya kikimuendea sawa. Michuano
hiyo inaendelea tena baadae kwa mchezo wa fainali kwa upande wa wanaume
ambapo Andy Murray wa Uingereza anayeshika namba mbili katika orodha za
ubora atachuana na Novak Djokovic wa Serbia anayeshika namba moja
katika orodha za ubora.