Sunday, July 7, 2013

STEWART HALL AMKUBALI KASEJA ASEMA BADO NI BONGE LA KIPA TZ"

Stewart hall akitabasamu kwa pozi la aina yake
Muingereza Stewart Hall Kocha  Mkuu wa Azam FC"bila kupepesa macho ametanabaisha kuwa Kaseja anastahili kuitwa tanzania one kutokana kuwa bado anauwezo mkubwa wa kulinda lango" Hall ameweka wazi na kusema kuwa kwa sasa sina mpango wa kusajili kipa mwingine kutokana na makipa niliyokuwa nao ambao ni Aishi Manula na Mwadini Ally" nataka hawahawa wapambane kuwania nafasi ya kipa namba moja wa azam fc" hivyo kwa msisitizo amesema sina mpango wa kusajili kipa mwingine.
Hall amesema kipa wake mwingine "Jackson Wandwi anafikiria kumpeleka kucheza kwa mkopo katika Club ya Ashanti United ya Ilala iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, ili kupata uzoefu baadaye arejee kushindana na Mwadini na Aishi.
Aidha Hall amesema nafahamu fika kuwa Kaseja ametupiwa virago MSimbazi na nasikia watu wanamzungumzia sana wakimhusisha na Azam fc. Mimi nakubali yule ni kipa mzuri na ana uzoefu. Ila mimi nina makipa wazuri wawili, Aishi na Mwadini. Nataka hawa washindane ili kumpata kipa nambari moja wa timu"
Hata hivyo Hall amesema kuwa bado Azam ina makipa wengine wazuri wa timu za vijana, ambao watakuwa wakipewa nafasi ya kujifua na kikosi cha kwanza msimu ujao.
“Hivyo nitakuwa na Aishi na Mwadini kama makipa wawili imara wa timu ya kwanza, maana yake Wandwi ataendelea kupoteza kiwango chake. hivyo nifikiria bora nimpeleke Ashanti ili akakuze kipaji chake na kupata  uzoefu, baadaye arejee kwenye timu akiwa imara zaidi".
Mbali na hilo tulipomuuliza kuhusu maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu tanzania bara na michuano ya kombe la shirikisho barani afrika Hall amesema kwamba Azam ambayo itaipeperusha bendera ya Tanzania kwa mara ya pili mfululizo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, iko katika mazoezi.
“Tunaendelea na mazoezi ya msimu mpya. Kwa sasa tupo katika programu ya ufukweni na gym. Baada ya hapo tutaanza programu rasmi ya uwanjani. Lakini wiki mbili za mwanzo za Agosti tutakwenda Afrika Kusini kuweka kambi,”.