Mshambuliaji nyota mahiri wa club ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametajwa katika orodha ya
wachezaji 10 watakaowania tuzo ya kiatu cha Dhahabu kwa mwaka 2013. Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa ureno atakuwa mchezaji wa kwanza wan chi hiyo
kushinda tuzo hiyo ambayo ilianza kutolewa mwaka 2003 mahsusi kwa
wachezaji waliozidi umri wa miaka 28. Mchezaji
mwenzake wa Madri Iker Casillas na kiungo mahiri wa Barcelona Andres
Iniesta ni miongoni wa nyota wengine walioteuliwa kugombea tuzo hiyo. Wachezaji
waliwahi kushinda tuzo hiyo ambayo hutolewa kwa kuangalia uwezo wake wa
kipindi chote alichocheza soka na kiwango chake cha sasa, ni pamoja na
Roberto Carlos, Ronaldinho, Francesco Totti na mshindi wa mwaka uliopita
Zlatan Ibrahimovic. Wachezaji
wanaweza kushinda tuzo hiyo mara moja pekee, ambapo sherehe zake
hufanyika jijini Monaco kila mwaka toka ilipoanzishwa. Mbali
na hao wengine waliokuwemo katika orodha ya mwaka huu ni pamoja na
Samuel Eto'o kutoka Anzhi Makhachkala, Andrea Pirlo anayekipiga
Juventus, Didier Drogba kutoka Galatasaray, Frank Lampard-Chelsea,
Miroslav Klose-Lazio, David Trezeguet-River Plate and David
Beckham-Paris Saint-Germain.