Mshambuliaji nyota wa
zamani wa Ufaransa, Thierry Henry ni moja kati ya wanadinga nyota 10
watakaounda kikosi kutoka katika Ligi Kuu ya Soka nchini Marekani-MLS
ambacho kitapambana na AS Roma ya Italia Julai 31 huko jijini Kansas. Henry
mwenye umri wa miaka 35 mshambuliaji wa klabu ya New York Red Bull
ambaye aliisadia Ufaransa kushinda Kombe la Dunia mwaka 1998, amefunga
mabao sita katika mechi 17 alizoichezea timu hiyo msimu huu. Kabla ya kwenda Marekani mwaka 2010 akitokea klabu ya Barcelona, henry amewahi kucheza katika vilabu vya Juventus na Arsenal. Golikipa
wa FC Dallas ambaye ni raia wa Peru Raul Fernandez, kiungo wa timu ya
taifa ya Canada Will Johnson na Beki wa Kansas City Aurelien Collin
ambaye ni raia wa Ufaransa ni miongoni mwa wachezaji wasiokuwa raia wa
Marekani walioteuliwa katika kikosi hicho cha nyota wa MLS.