MESSI RASMI ATARAJIWA KUREJEA BARCA MAZOEZINI JULAI 15
Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa argentina na club ya fc Barcelona, Lionel Messi anatarajiwa kurejea mazoezini Julai 15
baada ya kupumzika kwa wiki moja pekee katika likizo yake kutokana na
majukumu mbalimbali ambayo yamekuwa yakimtinga. Masimu
wa 2012-2013 kwa mchezaji huyo nyota ulimalizika Juni 15 baada ya
Argentina kuigaragaza Guatemala kwa mabao 4-0 katika mchezo wa kimataifa
wa kirafiki, hivyo kumanisha kwamba nyota huyo angekuwa na mwezi mzima
wa kupumzika kabla ya kuanza kwa msimu mpya. Hata
hivyo Messi mwenye umri wa miaka 26 alitumia nafasi hiyo kucheza mechi
mbalimbali za hisani kuzunguka dunia na kumaliza ziara yake hiyo
mwishoni mwa wiki iliyopita huko Chicago, Marekani. Jumla
ya ziara zote hizo Messi amesafiri kilimita zaidi ya 90,000 toka msimu
wa ligi ulipomalizika akitembelea nchi za Argentina, Ecuador, Guatemala,
Italia, Senegal, Colombia, Peru na Marekani. Nyota
huyo amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya msuli mwishoni mwa msimu
uliopita na mapumziko mafupi aatakayopata yatawapa uhakika mdogo
madaktari juu ya afya yake kabla ya kuanza msimu mpya wa 2013-2014.