FIFA-SEPP BRATTER ATARAJI KUZUNGUMZA NA MAOFISA WA ISRAEL
Bratter akiyatafakari mazungumzo
Sepp Blatter rais wa Shirikisho la
Soka Dunia-FIFA amemweleza kiongozi wa michezo nchini
Palestina kuwa atazungumza na maofisa wa Israel ili kujaribu kuondoa
vizuizi vya kusafiri walivyowekewa wachezaji wa taifa hilo. Blatter
alitarajiwa kukutana na ofisa mkuu wa soka nchini Israel kabla ya
kuzungumza na kiongozi wa kisiasa wan chi hiyo waziri mkuu Benjamin
Netanyahu kuzungumzia suala hilo. Palestina
wamekuwa wakichukizwa na vikosi vya usalama vya Israel ambavyo
vinalinda mji wa Gaza kuwazuia wanamichezo wa taifa hilo kusafiri kwa
uhuru katika pande hizo mbili. Blatter
amesema atakwenda Israel sio kwenda kukitetea Chama cha Soka cha
Palestina lakini pia kutetea misingi ya kanuni za FIFA ambayo ni
kuunganisha watu na sio kuwagawa.