LIVERPOOL YAIBWAGA CHINI OFA YA ARSENAL KUHUSU SUAREZ
Majogoo wa jiji london Club ya soka ya Liverpool
imepiga chini ofa ya paundi milioni 30 waliyotoa Arsenal kwa ajili ya
kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo Luis Suarez. Kumekuwa
na tetesi za muda mrefu za Suarez kutaka kuuzwa baada ya kufungiwa
mechi 10 kwa kumng’ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic katika Uwanja
wa Anfield msimu uliopita. Klabu
ya Real Madrid ya Hispania ndio wanaotegemewa kumsajili mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Uruguay baada ya kutamka wazi kwamba ameyachoka
maisha ya Uingereza. Mwishoni
mwa wiki hii Arsenal nao walidaiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha
kumuwania lakini Liverpool walikataa kutoa kauli yoyote kuhusiana na
tetesi hizo huku wakisisitiza kwamba bado wanamhitaji mshambuliaji huyo.