Kiungo mahiri wa
kimataifa wa Brazil, Luiz Gustavo anatarajiwa kukubali uhamisho wake
kwenda Arsenal ili aweze kucheza zaidi katika kikosi cha kwanza kwa
ajili ya michuano ya Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil. Kiungo
huyo mkabaji wa Bayern Munich ambaye amejikuta akishindwa kupata namba
ya moja kwa moja katika kikosi cha kwanza anakaribia kukamilisha usajili
wake wa paundi milioni 14 kwenda Emirates wiki hii. Gustavo
anaamini kuwa nafasi yake itazidi kuwa finyu chini ya kocha mpya Pep
Guardiola ambaye ameonyesha kumtumia sasa Javi Martinez ambaye naye
anacheza nafasi hiyo ndio maana anaona uhamisho wake kwenda Arsenal
unaweza kumsadia. Akihojiwa
jijini Basel kabla ya mchezo wa kirafikiwa kimataifa baina ya Brazil na
Switzerland kesho, Gustavo amesema mkataba wake na Bayern unamalizika
2015 lakini ni muhimu kwake kucheza katika kikosi cha kwanza ili aweze
kuitwa katika timu ya taifa.